MGOMBEA WA CHADEMA AWEKWA CHINI YA ULINZI NA POLISI




Mgombea udiwani kwa tiketi ya Chadema Kata ya Sofi wilayani Malinyi, mkoani Morogoro Riko Venance amewekwa chini ya ulinzi na polisi wakati akitembelea kituo cha kupigia kura cha Shule ya Msingi Mission leo Jumapili Novemba 26,2017.

Mwenyekiti wa Chadema Kanda ya Kati, Alfonce Mbassa amesema bado hawajaambiwa kwa nini mgombea huyo anashikiliwa na polisi wakati sheria inamruhusu kutembelea vituo.

"Nimepewa taarifa kwamba mgombea wetu anashikiliwa na polisi na hivi ndio naelekea eneo la tukio, bado sijajua kwa nini amewekwa chini ya ulinzi, nitatoa taarifa baadaye," amesema Mbassa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro hajapatikana kuzungumzia tukio hilo, jitihada za kumtafuta bado zinaendelea.

Kata ya Sofi ina vijiji vitatu ambapo viwili vinaongozwa na Chadema na kimoja hakina uongozi kwani kilishindwa kufanya uchaguzi kutokana na migogoro ya mipaka.

Kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2012 kata hiyo ilikuwa na wakazi 12,000 huku waliojiandikisha kupiga kura mwaka 2014/15 wakiwa 8,700.

By Amina Juma, Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post