Robert Mugabe anatarajiwa kuhudhuria kuapishwa kwa rais mpya wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa kulingana na runinga ya habari ya taifa hilo ZBC .
Maandalizi yameanza katika uwanja wa kitaifa wa michezo katika mji mkuu wa Harare ambapo hafla hiyo itafanyika.
Mwandishi wa masuala ya kidiplomasia Judith Makwanya amesema kuwa kiongozi anayeondoka anatarajiwa kukagua gwaride akitoa kwa heri huku kiongozi mpya akilijulisha jeshi katika sherehe hiyo ya gwaride.
Tayari waziri wa Uingereza barani Afrika Rory Stewart amewasili nchini Zimbabwe mapema kulinga na chombo cha habari cha AFP.
Afisa huyo amewasili tayari kuhudhuria kuapishwa kwa rais mpya siku ya Ijumaa.
Bwana Sterwart anatarajiwa kukutana na viongozi wa kisiasa na wale wa kibiashara pamoja na makundi ya haki za kibinaadamu na mashirika yasiokuwa ya kiserikali kulingana na waziri wa maswala ya kigeni nchini Uingereza.
Ametaja mabadiliko hayo ya kihistoria kuwa wakati muhimu baada ya utawala mbaya wa rais wa zamani Robert Mugabe.
Uingereza inataka kuwa mshirika wa kweli wa raia wa Zimbabwe wakati huu ambao wanaanza mwanzo mpya, bwana Stewart aliambia AFP
Chanzo- BBC
Social Plugin