Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ALIYEKUWA KAMPENI MENEJA WA KATAMBI..SASA MWENYEKITI WA BAVICHA SHINYANGA MJINI KESHO KUFICHUA MAZITO KUHUSU KATAMBI KUHAMIA CCM



Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) wilaya ya Shinyanga Mjini Samson Ng’wagi ameeleza kusikitishwa na kitendo cha aliyekuwa mwenyekiti wa baraza la vijana Chadema taifa Patrobas Katambi kujiondoa Chadema na kuhamia CCM huku akiwapachika jina la ‘Makarai’ vijana wa Chadema.

Kufuatia kitendo hicho alichokiita kuwa ni usaliti kwa CHADEMA,Ng’wagi ambaye alikuwa Kampeni Meneja wa Katambi alipogombea ubunge jimbo la Shinyanga mjini katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015, amesema kesho Alhamis Novemba 23,2017,saa tano asubuhi atamwaga upupu wote kuhusu Katambi.

Ng’wagi ameiambia Malunde1 blog kuwa kesho atafanya kikao na waandishi wa habari ili kuueleza umma wa watanzania jinsi Katambi alivyouhadaa umma kuwa amehamia CCM kwa nia njema.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com