Kikao cha Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) kimeridhia kumpokea aliyekuwa Mwenyekiti wa Wanawake CCM (UWT), Sophia Simba baada ya kuomba radhi na kuomba kurejea CCM baada ya kufukuzwa uanachama.
Sophia Simba alifukuzwa na chama hicho baada ya kubainika kukisaliti chama hicho kwa kumuunga mkono Edward Lowassa ambaye sasa ni kada wa CHADEMA.
Akiongoza kikao hicho leo Jumanne Novemba 21,2017,Mwenyekiti wa CCM taifa Dkt. John Pombe Magufuli amesoma barua ya Sophia kuomba radhi mbele ya kikao cha halmashauri kuu ya CCM (NEC) na kuwahoji wajumbe kama wanakubali kumsamehe jambo lililokubaliwa.
"MwanaCCM aliyefukuzwa uanachama amekuwa akiandika barua nyingi za kuomba radhi lakini tumekuwa tukinyamaza, kikao hiki ndiyo kilimfukuza," amesema Magufuli.
Sophia Simba aliandika barua za kuomba kusamehewa baada ya kukiri makosa yake na kwamba yeye amekulia ndani ya CCM hivyo hajisikii kuishi nje ya chama hicho.
Baada ya kuwahoji wajumbe na kukubaliwa Magufuli aliandika kwenye barua hiyo kuwa amekubaliwa kurudi CCM.
Social Plugin