Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Jumamosi Novemba 4,2017 amefungua mkutano mkuu wa wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) mwaka 2017.
Mkutano huo mkuu wa SPC ulikuwa na lengo la kujadili masuala mbalimbali ya kujenga klabu na masuala kadha kadha kuhusu tasnia ya habari.
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika katika ukumbi wa Katemi Hotel mjini Shinyanga,Matiro alisema kalamu ya mwandishi wa habari ni fimbo hivyo kuwataka wazitumie vyema kwa ajili ya maendeleo katika jamii.
Alisema kutokana na kwamba waandishi wa habari ni wadau wakubwa wa maendeleo ni vyema wakawa wazalendo kwa kutangaza fursa za maendeleo katika mkoa wa Shinyanga.
“Serikali inatambua mchango wa waandishi wa habari,naomba tushirikiane katika kuwaletea maendeleo wananchi,sisi viongozi wa serikali tutaendelea kuwahamasisha wakurugenzi katika halmashauri za wilaya kuwapa taarifa sahihi pale mnapohitaji”alieleza Matiro.
Katika hatua nyingine aliwaasa waandishi wa habari kujiendeleza kielimu ili kuongeza umahiri na ufanisi katika kazi zao lakini pia kukabiliana na sheria ya huduma za habari ya mwaka 2016 inayotaka mwandishi wa habari awe na kiwango cha elimu kuanzia ngazi ya diploma.
Matiro aliwasisitiza waandishi wa habari kuandika habari za maendeleo ya mkoa wa Shinyanga huku akiwaomba kutangaza fursa za uwekezaji katika viwanda kuunga mkono jitihada za serikali katika kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda.
“Tutakuwa na kiwanda cha nyama katika manispaa ya Shinyanga hivi karibuni,kutokana na kuwa na kiwanda hicho kinahitajika kiwanda kingine cha ngozi,naomba wadau kuja kuwekeza katika kiwanda cha ngozi”,aliongeza.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde waandishi wa habari mkoani humo wanaunga mkono jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Mheshimiwa rais Dkt. John Pombe Magufuli katika kuwaletea maendeleo wananchi.
“Waandishi wa habari ni daraja kati ya serikali na wananchi,hivyo kupitia kalamu zetu tupo tayari na tumekuwa tukishirikiana na viongozi wa serikali kufanikisha utekelezaji wa sera mbalimbali ikiwemo hii ya kujenga uchumi wa viwanda”,alisema Malunde.
“Ili kufanikisha haya,waandishi wa habari tunaomba ushirikiano kutoka katika mamlaka mbalimbali zinazohusika kwani baadhi ya viongozi wa serikali hawapendi kushirikisha vyombo vya habari katika kutekeleza mambo yanayogusa jamii”,aliongeza.
Aidha Malunde aliwataka waandishi wa habari kufanya kazi kwa kuzingatia maadili ya uandishi wa habari na sheria mbalimbali ikiwemo Sheria ya huduma za habari mwaka 2016 ambayo imekuwa mwiba kwa uhuru wa vyombo vya habari.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Viongozi wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Mwenyekiti Kadama Malunde (wa pili kutoka kushoto,akifuatiwa na Katibu Mtendaji Stephen Wang'anyi na katibu Msaidizi Ali Lityawi) wakimpokea mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro (kushoto) ili kushiriki katika mkutano mkuu wa SPC,2017 uliofanyika katika ukumbi wa Katemi Hotel Novemba 4,2017.Picha zote na Patrick Mabula na Frank Mshana - Shinyanga Press Club
Mgeni rasmi wakati wa mkutano mkuu wa wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) mwaka 2017,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza wakati wa kufungua mkutano huo
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro akizungumza katika mkutano huo.Wa kwanza kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Shaaban Alley na katibu mtendaji wa SPC,Stephen Wang'anyi wakimsikiliza mkuu huyo wa wilaya.
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akitoa hotuba fupi wakati wa mkutano mkuu wa wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (Shinyanga Press Club – SPC) mwaka 2017.Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro.Kulia ni Katibu Msaidizi wa SPC,Ali Lityawi
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akiwasisitiza waandishi wa habari kuzingatia maadili ya uandishi wa habari na kutoogopa kufichua maovu yanayofanyika katika jamii
Wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ukumbini
Katibu Mtendaji wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Stephen Wang'anyi akisoma taarifa ya mafanikio ya klabu hiyo tangu mwaka 2015 mpaka Oktoba 31,2017
Wanachama wa SPC,Kareny Masasy na Marco Mipawa (kushoto) wakifuatilia yaliyokuwa yanajiri ukumbini
Wanachama wa SPC wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde akitoa neno wakati wa majadiliano ya ajenda mbalimbali wakati wa mkutano huo.Kulia ni Mweka Hazina wa SPC,Stella Ibengwe.
Wanachama wa SPC wakiwa ukumbini
Mkutano unaendelea
Wanachama wa SPC,Shaban Njia (kushoto) na Chibura Makorongo wakiwa ukumbini
Mratibu wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Nunu Abdul akiwa ukumbini
Mwanachama wa SPC,Jennifer Mahesa akifurahia jambo ukumbini
Mwanachama wa SPC,Stephen Kidoyayi akiwa ukumbini
Wananchama wa SPC wakiwa ukumbini,Lucy Masalu (kushoto) na Annastazia Paul wakiwa ukumbini
Mwanachama wa SPC,Zuhura Waziri akitafakari jambo ukumbini
Picha ya pamoja,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro na wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga (SPC) wakati wa mkutano mkuu wa SPC 2017
Picha ya pamoja, mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro na wanachama wa SPC
Picha ya pamoja
Picha ya pamoja mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro na baadhi ya wajumbe wa kamati ya utendaji ya SPC
Picha ya pamoja, mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro (katikati),Mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Kadama Malunde (kulia) na Katibu Mtendaji wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga,Stephen Wang'anyi
Picha ya kumbukumbu,mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na baadhi ya wanachama wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga.
Picha zote na Patrick Mabula na Frank Mshana - Shinyanga Press Club
Social Plugin