RAIS MAGUFULI AIANDIKIA BARUA CANADA BAADA YA KUCHOKA KUSUBIRI BOMBADIER


Rais John Magufuli amemwandikia barua waziri mkuu wa Canada kuulizia kuhusu ndege ya Bombadier, inayoshikiliwa nchini humo na kumtaka ashughulike suala hilo kwa haraka.


Akizungumza katika uzinduzi wa Uwanja wa ndege mjini Bukoba Jumatatu Novemba 6, Rais Magufuli amesema amemtuma pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali, George Masaju kwenda Canada kushughulikia suala hilo kisheria.


"Nimemwandikia barua waziri wa Canada kuulizia kwanini ndege yetu inakaa zaidi ya miezi sita, tumechoka kusubiri. Nimemtuma pia mwanasheria mkuu ili akapambane nao kisheria," amesema.


Amesisitiza kwamba kama wameamua kupambana kisheria watapambana na amewataka wanasheria wa Tanzania kushikamana ili kuhakikisha kwamba ndege hiyo inakuja Tanzania.


Rais Magufuli amewaonya wananchi pia kuacha kuzungumza kwenye mitandao ya kijamii. Alisema “ninawaomba watu wa vyama vyote waunge mkono juhudi hizi zinazofanywa na serikali.”


Magufuli ambaye ametimiza miaka miwili tangu achaguliwe kuwa Rais wa Tanzania amesema ndege zote sita zilizonunuliwa na Serikali zitakuja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post