Emmerson Mnangagwa ameapishwa kuwa rais mpya wa Zimbabwe. Maelfu ya Wazimbabwe waliojaa furaha na matumaini wamejazana kwenye uwanja mkuu wa michezo mjini Harare kushiriki katika sherehe za kuapishwa rais mpya.
Emmerson Mnangagwa ni rais wa pili, baada ya Robert Mugabe kuitawala nchi hiyo tangu Zimbabwe ilipojipatia rasmi uhuru wake mwaka 1980.
Viongozi kadhaa wa Afrika, wakiwemo wale wa Botswana, Msumbiji na Zambia, wanahudhuria sherehe za kuapishwa Mnangagwa.
Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini amelazimika kusalia Pretoria kwa mazungumzo pamoja na rais mpya wa Angola.
Mugabe aliyeitawala Zimbabwe kwa mkono wa chuma kwa muda wa miaka 37 hahudhirii sherehe hizo.
Gazeti la seikali, The Harald, linasema Mnangangwa na Mugabe wamekubaliana asihudhuirie sherehe hizo na kwamba amemhakikishia rais huyo mkongwe, kwamba yeye, mkewe Grace na familia yake yote hawatoandamwa kisheria.