Serikali kupitia mamlaka zake imezifungia rangi za midomo zinazozalishwa na Mwanadada aliyewahi kuwa Miss Tanzania na Muigizaji wa Filamu, Wema Sepetu. Rangi hizo zinajulikana kwa jina la "Kiss".
Kwa mujibu wa taarifa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) pamoja na Shirika la Viwango Nchini(TBS) wamebaini kuwa rangi hizo hazina ubora kwa matumizi ya binadamu.
Kwa upande wa Meneja wa Wema Sepetu, Happy Shame alipotakiwa kuzungumzia suala hilo amefunguka na kusema kwamba taarifa za kufungiwa kwa bidhaa hizo yeye kama Meneja hajazipata bali anachofahamu mzigo ulikuwa haujaingia sokoni na kwamba muigizajin huyo alikuwa bado akifuatilia vibali kutoka mamlaka husika.
Rangi hizo za mdomo za muigizaji Wema Sepetu zilizinduliwa kwa mara ya kwanza mwaka 2015 usiku wa birthday yake.
Social Plugin