Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe amewahamasisha wazee kuanzia umri wa miaka 60 na kuendelea kujitokeza kwenye zoezi la upigwaji picha ili waweze kupatiwa kadi za bima ya afya zitakazowawezesha kupatiwa matibabu bure kwenye zahanati, vituo vya afya na hospitali.
Hayo ameyazungumza mara baada kuwasili katika Ofisi za Mtendaji Kata ya Kabuku Nov 23, 2017 kuhamasisha huduma za afya.
Hatua hiyo ni muendelezo wa agizo la serikali ya awamu ya tano ya rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kuhakikisha wazee kuanzia umri wa miaka 60 na kuendelea wanapatiwa matibabu bure. PICHA/HABARI NA KAJUNASON/MMG -KABUKU, HANDENI.
Diwani wa Kata ya Kabuku, Amina Mnegelo akizungumza machache mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe huku wazee wakimfuatilia kwa makini.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akisalimiana na wazee wa kata ya Kabuku baada ya kuwasili katika ofisi ya mtendaji kuzungumza na wazee juu ya mpango wa kuwapatia kadi za bima ya afya zitakazowawezesha kupatiwa huduma ya afya bure katika Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali. Mkutano ulifanyika katika Ofisi za Mtendaji Kata ya Kabuku Nov 23, 2017.
Wazee wakimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe.
Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Godwin Gondwe akiwasikiliza wazee wa Kata ya Kabuku.
Social Plugin