Kimemtua aliyekuwa makamu wa rais Emmerson Mnangagwa ambaye alifutwa wiki mbili zilizopita kama kiongozi wake.
Kufutwa kwa Bw. Mnangagwa kumezua mambo mengi huku jeshi likitwaa madaraka na kumzuia Mugabe 93, kumteua mke wake Grace kama makamu wa rais.
Maelfu ya watu nchini Zimbabwe waliingia barabarani siku ya Ijumaa kuandamana kumpinga Bw. Mugabe.
Bw. Mugabe anatarajiwa kukutana na makanda wa jeshi na msafara wa magari umeonekana ukiondoka makao ya rais.
Mkuu wa chama chenye nguvu cha wale waliopigania uhuru Chris Mutsvangwa, aliiambia Reuters kuwa chama kilikuwa kinaanza mchakato wa kumuondoa Mugabe madarakani kama rais.
Maelfu ya raia wa Zimbabwe jana walijitokeza barabarani hasa mjini Harare katika jitihada za kuongeza shinikizo za kumtaka rais Mugabe ajiuzuulu,wakishikilia mabango yaliyoandikwa Mugabe Must Go.
Zanu-PF ndio chama kilichomsaidia Mugabe kuwa madarakani nchini kwa takriban miaka 40.Maelfu ya raia wa Zimbabwe jana walijitokeza barabarani hasa mjini Harare katika jitihada za kuongeza shinikizo za kumtaka rais Mugabe ajiuzuulu
Lakini sasa inabidi wamshinikize ajiuzulu kufuatia mpasuko mkubwa katika chama tawala.
Jeshi la nchi hiyo lilichukua hatamu za kiserikali na kumweka Mugabe chini ya kizuizi cha nyumbani tangu juzi na wamekuwa wakifanya mazungumzo ya kina.
Mugabe angependelea mkewe kumrithi lakini wapiganiaji wa uhuru nchini humo wanamtaka aliyekuwa makamu wa Rais Emmerson Mnangagwa ambaye Mugabe alimfuta kazi wiki iliyopita, kutokana na uhasama mkubwa baina yake na mkewe rais Mugabe uliotokana na upiganiaji huo wa madaraka.
Chanzo- BBC