Maandamano hayo yanajiri kufuatia furaha ilioonekana miongoni mwa raia baada ya jeshi kuingilia kati na kumzuia rais Mugabe kwa muda nyumbani kwake siku ya Jumatano.
Wanajeshi katika ikulu ya Whitehouse walioonekana wakiwarudisha nyuma waandamanaji.
Jeshi liliingilia kati baada ya rais Mugabe kumfuta kazi makamu wake wa urais , akionyesha ishara za kutaka mkewe kumrithi.
Bwana Mugabe , mwenye umri wa miaka 93 ameiongoza Zimbabwe tangu ilipojipatia uhuru kutoka kwa Uingereza 1980.
Jeshi limehakikisha kuwa anaendelea kukaa katika makoa yake huku likidai kujadiliana naye na kwamba litatangaza kwa wananchi matokeo ya mazungumzo hayo hivi karibuni.
Mkutano wa siku ya Jumamosi unaungwa mkono na jeshi na wanachama wa chama cha Zanu -PF.
Chanzo-BBC