Afisa uhusiano na mawasiliano,Ofisi ya mratibu mkazi mashirika ya umoja wa mataifa(UN) Didi Nafisa akitoa mada leo Jumatatu Novemba 27,2017 kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) juu mradi wa pamoja wa Kigoma unaofanywa na mashirika 16 ya umoja wa mataifa katika kambi za wakimbizi zilizopo mkoani Kigoma.
Waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari wanashiriki katika mafunzo hayo ya siku mbili kuhusu kuripoti habari za wakimbizi na umakini dhidi ya changamoto ya uwepo wa sheria mpya ya habari.Mafunzo hayo yanayofanyika katika ukumbi wa Nzimano Kigoma Mjini yameandaliwa na shirika la umoja wa mataifa(UN)na kuratibiwa na MISATAN Tanzania.Picha zote na Editha Karlo - Kigoma
Kaimu Mkurugenzi MISATAN Tanzania Gasirigwa Sengiyumva akisisitiza jambo kwa washiriki wa mafunzo hayo
Waandishi wa habari wa Mkoa wa Kigoma kutoka vyombo mbalimbali wakiwa kwenye mafunzo ya siku mbili kuhusu kuripoti habari za wakimbizi na umakini dhidi ya changamoto ya uwepo wa sheria mpya ya habari mafunzo yaliyoandaliwa na shirika la umoja wa mataifa(UN)na kuratibiwa na MISATAN Tanzania