Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Kituo cha Nansio wilayani Ukerewe, John Kalongola amejinyonga kwa kipande cha chandarua nyumbani kwake.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi amesema mwili wa askari huyo umehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ukerewe.
Amesema baada ya uchunguzi na utaratibu kukamilika mwili utasafirishwa kwa mazishi mkoani Iringa.
Kamanda Msangi amesema mwili huo ulibainika baada ya harufu kutoka ndani ya nyumba yake na mlango ulipovunjwa ulikutwa ukining’inia.
Mwili wa askari huo uligunduliwa jana Ijumaa Desemba 29,2017. Amesema kipande cha chandarua kilifungwa juu ya dari.
Social Plugin