Askofu mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship (FGBF) Zakaria Kakobe, amesema hahofii kuchunguzwa na serikali kuhusiana na ukwasi anaoumiliki na kuongeza kuwa fedha alizonazo ni zaidi ya fedha zinazomilikiwa na serikali nyingi duniani.
Akizungumza wakati wa ibada ya Jumapili kanisani hapo leo Askofu Kakobe amesema hana wasiwasi wa kuchunguzwa utajiri wake na kuongeza kuwa kwa sasa anamiliki pesa nyingi zaidi ya serikali za China na Marekani.
Pia, alitumia fursa hiyo kuwajibu watu wote waliokuwa wakihoji uraia wake.
" Wanaosema Kakobe amekimbia nchi nawashangaa sana nipo na wala siendi popote, kipindi Fulani walikuja kuchunguza uraia wangu lakini wakaambulia patupu, tutabanana hapa hapa.
" Watu wanasema Niko kimya sana wala sipo kimya tatizo wanataka nizungumze wanayoyataka wao, sasa Mimi sio mtu wa namna hiyo, ukiniona nimesimama katika madhabahu Haya basi ujue nina kibali cha Mungu, mtu ukiitwa Mbwa kwani wewe ndiyo utakuwa Mbwa? Sasa nashangaa unaogopa nini kuitwa Mbwa wakati wewe sio Mbwa" -Kakobe
Akihubiri wakati wa mkesha wa sikukuu ya Krismasi wiki iliyopita, askofu huyo alisema yeye ni tajiri zaidi ya serikali ya Tanzania.
Katika mahubiri ya leo, Askofu Kakobe amewaambia waumini wake kuwa utajiri anaomiliki kwa sasa ni zaidi ya serikali nyingi duniani.
Social Plugin