Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi CCM Dkt. John Pombe Magufuli amesema hana mpango wa kubadilisha Sekretarieti ya chama hicho na itaendelea kama ilivyo chini ya Katibu Mkuu Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti huyo mpya alichaguliwa kwenye mkutano wa tisa wa chama hicho uliomalizika leo jioni mjini Dodoma kwa kupata kura zote 1821 za wajumbe wa mkutano mkuu.
Rais Magufuli atahudumu katika nafasi hiyo kwa miaka mitano kuanzia jana hadi mwaka 2022 utakapofanyika uchaguzi mwingine.
Katika hotuba yake baada ya kuchaguliwa Dkt. Magufuli alisema kwa sasa hana mpango wa kubadilisha Sekretarieti na itaendelea kama ilivyo chini ya katibu mkuu wa Chama hicho Ndugu Abdulrahman Kinana.
Matokeo ya Uchaguzi huo yalitangazwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai ambaye aliwataja washindi wote katika nafasi za Mwenyekiti Taifa, Mwenyekiti Zanzibar na Makamu Mwenyekiti Taifa.
Mbali na Mwenyekiti wa Taifa lakini pia Rais wa Zanzibar Dkt. Ali Mohamed Shein alishinda nafasi ya Mwenyekiti wa CCM Zanzibar kwa kura zote 1821 wakati Ndugu Philip Mangula akishinda nafasi ya Makamu mwenyekiti Taifa kwa kura zote 1821.
Miongoni mwa wajumbe hao waliopigiwa kura , Stephen Wasira ameongoza kwa ushindi baada ya kujikusanyia kura 1505 kati ya kura halali 1779.
Wajumbe 15 waliochaguliwa ni,
1. Steven Wassira
2. Jerry Silaa
3. Dr Fenera Mukangara
4. Angel Akilimali
5. Jackson Msome
6. Dr Ibrahim Msengi
7. Theresia Mtewele
8. Mwantumu Zodo
9. Ernest Sungura
10. Deougratius Ruta
11. Eng Burton Kihaka
12. William Sarakikya
13. Richard Charles
14. Anna Msuya
15. Charles Shanda
Social Plugin