Shirika la Kivulini limeendesha mafunzo ya kuboresha mfumo wa rufaa kwa watoa huduma mbalimbali kwa lengo la kujadili namna ya kutoa rufaa kuwasaidia wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.
Mafunzo hayo yamefanyika leo Jumatano Disemba 6,2017 katika ukumbi wa mikutano wa Empire Hotel mjini Shinyanga ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia na watoto yaliyoanza Novemba 25,2017 na yatafikia kilele chake Disemba 10 mwaka huu.
Miongoni mwa washiriki katika mafunzo hayo ni maafisa maendeleo ya jamii,afya,jeshi la polisi,dawati la jinsia watendaji wa vijiji,wenyeviti wa vijiji,wajumbe wa baraza la ardhi,viongozi wa jeshi la jadi sungusungu na wazee maarufu.
Afisa mwandamizi wa mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana Bi. Eunice Mayengela alisema washiriki wa mafunzo hayo wanatoka vijiji vitano vya halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Shinyanga Vijijini) ambavyo ni Nyida,Nsalala,Butini,Nduguti na Welezo ambako mradi huo unatekelezwa.
Mayengela alisema lengo la mafunzo hayo ni kuboresha mfumo wa kutoa rufaa ili kuwasaidia wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia ili waweze kupata huduma kutoka kwa viongozi wa maeneo wanakotoka.
Afisa mradi huyo alisema watu wengi katika jamii wamekuwa wakishindwa kutafuta msaada kwa vitendo vya kikatili wanavyofanyiwa kutokana na aibu,unyanyapaa,hofu ya kupoteza ndoa zao na wengine kuwa na mashaka ya kutosaidiwa hivyo kuwataka kujiamini ili kuhakikisha vitendo hivyo vinakomeshwa katika jamii.
Naye Mzee maarufu kutoka kijiji cha Butini,Joseph Maganga alisema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake vinazidi kupungua kutokana na jamii kupewa elimu kuhusu madhara ya ukatili.
Hata hivyo Mwenyekiti wa kijiji cha Nyida, Peter Nkoba alisema pamoja jitihada wanazofanya katika kuielimisha jamii kuachana na vitendo vya kikatili bado baadhi ya akina baba wananyanyasa wake zao hasa baada ya kipindi cha mavuno na wakati wa kilimo wanashiriki wote katika uzalishaji mali.
Kwa upande wake afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Deus Masili Muhoja aliliomba jeshi la jadi sungusungu kuongeza katika majukumu yake suala la kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Naye Mwakilishi wa Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga,Joseph Christopher alisema mtu yeyote aliyefanyiwa ukatili wa kijinsia hapaswi kutozwa pesa yoyote hivyo kuwataka wananchi kutoa taarifa pale inapotokea wanaombwa pesa za mafuta na viongozi kwenye maeneo yao.
“Utaratibu wa wananchi kutoa pesa kwa wananchi haupo,kama ni utaratibu basi wangekuwa wanatoa risti,wanaofanya hivyo ndiyo wanachangia kuharibu sifa ya jeshi la polisi”,aliongeza.
ANGALIA PICHA ZA MATUKIO WAKATI WA MAFUNZO HAYO
Afisa mwandamizi wa mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana Bi. Eunice Mayengela akizungumza wakati wa mafunzo ya kuboresha mfumo wa rufaa kwa watoa huduma mbalimbali kutoka halmashauri ya wilaya ya Shinyanga leo Jumatano,Disemba 6,2017.Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Bi. Eunice Mayengela akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Mwenyekiti wa kijiji cha Nsalala Sandeco Ndegelege akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo ambapo alisema vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake vinaendelea kupungua katika jamii kutokana na jamii kupewa elimu kuhusu madhara ya ukatili.
Afisa mwandamizi wa mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana Bi. Eunice Mayengela akitoa mada wakati wa mafunzo hayo.
Washiriki wa mafunzo hayo wakifuatilia mada ukumbini
Mwakilishi wa Jeshi la Polisi wilaya ya Shinyanga,Joseph Christopher akizungumza wakati wa mafunzo hayo.
Afisa maendeleo ya jamii kata ya Nyida Suzana Chami akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo
Washiriki wa mafunzo hayo wakiwa ukumbini
Mzee maarufu kutoka kijiji cha Butini,Joseph Maganga akichangia hoja wakati wa mafunzo hayo
Mwenyekiti wa dawati la jinsia na watoto jeshi la polisi wilaya ya Shinyanga,Mkaguzi msaidizi wa polisi,Zainab Mangala akizungumza katika mafunzo hayo.
Afisa mtendaji wa kijiji cha Nguduti Evarist Kabuga akizungumza ukumbini
Mafunzo yanaendelea
Kaimu mkuu wa kituo cha polisi Shinyanga,Inspekta Jeremiah Zitta akisisitiza jambo ukumbini
Kamanda wa jeshi la jadi sungusungu kata ya Nsalala,John Machiya akichangia hoja ukumbini
Tunasikiliza hoja ya mjumbe....
Washiriki wa mafunzo hayo wakisikiliza hoja ya Kamanda wa jeshi la jadi sungusungu kata ya Nsalala,John Machiya
Mafunzo yanaendelea
Afisa Maendeleo ya jamii kata ya Nsalala,Beatrice Macha akizungumza ukumbini
Askari polisi (WP) Swaiba Msangi kutoka kitengo cha upelelezi jeshi la polisi Shinyanga akizungumza wakati wa mafunzo hayo
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Deus Masili Muhoja akichangia hoja ukumbini.
Afisa mwandamizi wa mradi wa usawa wa kijinsia kujenga uwezo kiuchumi kwa wanawake na vijana Bi. Eunice Mayengela akionesha vipeperushi vya hadithi za watu waliofanyiwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Washiriki wa mafunzo hayo wakisoma hadithi ya ukatili wa kijinsia
Washiriki wakisoma hadithi za watu waliofanyiwa ukatili wa kijinsia.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog