Rais na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) John Pombe Magufuli ameuambia Mkutano Mkuu wa CCM kuwa kuna idadi kubwa ya wanachama wa vyama vya upinzani ambao wanataka kujiunga na CCM.
Tayari Wabunge wawili wa upinzani, Maulid Mtulia (Kinondoni-CUF) na Godwin Molel (Siha-Chadema) wamejiuzulu nafasi zao na kujiunga CCM.
Akihutubia Mkutano Mkuu wa CCM leo, Jumatatu Desemba 18 Rais Magufuli amesema kuna mbunge mwengine wa upinzani anataka kujiunga na CCM pamoja na madiwani wa kata zake 8.
“Hiki ni kimbunga, na wataisoma namba," amesema Rais Magufuli.
Magufuli pia amewataka viongozi wa CCM ambao wamechaguliwa hivi karibuni kuhakikisha kuwa jukumu lao la kwanza ni kuongeza idadi ya wanachama, ili ikifika uchaguzi ujao washindani wao wasiambulie chochote.
Social Plugin