MAKAMU WA CHUO CHA IJA ASHINDA KUKU LUSHOTO KATIKA BONANZA


Fahamu Mtulya Mshindi wa kuku (Naibu Mkuu wa Chuo Taaluma
Nazael Mkumbo Mshindi wa kuku

Makamu Mkuu wa Chuo cha uongozi wa mahakama IJA, Fahamu Mutlya mwishoni mwa wiki alionesha uhodari wa kukimbia baada ya kufanukiwa kumkamata kuku katika bonanza kuadhimisha siku ya uhuru na kufunga mwaka wa 2017 lililofanyika katika uwanja wa chuoni hapo.


Mtulya aliweza kuwashinda wengine waliokuwa kwenye kundi la wahadhiri baada ya kuchomoka kwa haraka na kisha kumdaka kuku huyo wakati kundi la uhasibu mshindi alikuwa Noel Njau wakati Barnaba john alishinda kundi la utawala.

Mpira wa kikapu watumishi waliweza kuwafunga wanafunzi wa chuoni hapo magoli 12 -8 na mpira wa wavu watumishi walifungwa seti 3-2.

Mwenyekiti wa kamati ya Bonanza hilo,Daudi Hemba alisema lilifanyika kwa lengo la kuwaeka pamoja watumishi na wanafunzi katika kujenga afya zao huku wakitafakari kuhusu mambo mbalimbali yahusuyo uhuru wa nchi hii.

“Bonanza hili limefanyika kwa lengo la kuwaweka pamoja watumishi na wanafunzi lakini pia kujenga afya zao huku wakitafakari kuhusu uhuru”alisema Hemba.

Mkuu wa Chuo cha IJA,Paul Kihwelo aliwataka watumishi kujenga tabia ya kufanya mazoezi ya mara kwa mara ili kuimarisha afya zao.

“Bila shaka mnafahamu kwamba anayeshiriki michezo si rahisi kushambuliwa na magonjwa mbalimbali,na ndiyo maana tumeanzisha IJA joging club ambayo watumishi na wanafunzi wanashiriki kila jumamosi”alisema Kihwelo.


Katika bonanza hilo pia lilifanyika zoezi la upimaji wa afya
ambapo watu 25 waliojitokeza kupima virusi vya ukimiwi walionekana kutokuwa na maambukizi wakati waliopima kisukari (Blood Suger) walikuwa 30 ambao walionekana kuwa ya kawaida.

Habari kwa Hisani ya Blog ya
Kijamii ya Tanga Raha 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post