Msichana aliyejulikana kwa jina la Habibu Abuu (21) mkazi wa mtaa wa Bukondamoyo wilayani Kahama mkoani Shinyanga amemwagiwa maji ya moto maeneo ya sehemu zake za siri na tumboni na kumpiga akituhumiwa kujihusisha na imani za kishirikina.
Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa tukio hilo limetokea jana Ijumaa Disemba 15,2017 majira ya saa mbili usiku katika mtaa huo.
Inaelezwa kuwa watuhumiwa waliomwagia maji hayo kuwa ni Festo Masanja (37) na Yohana Cprian (23) ambao tayari wanashikiliwa na jeshi la polisi.
Habari kutoka eneo la tukio zinasema chanzo cha tukio hilo ni Habibu Abuu kujihusisha na masuala ya imani za kishirikina na kufanya kumloga mama mzazi wa watuhumiwa hao wawili.
Habiba Abuu amelazwa katika hospitali ya wilaya ya Kahama kwa kwa ajili ya matibabu.
Chanzo-Malunde1 blog
Social Plugin