Mbunge Nape Nnauye ametoa yake ya moyoni kwa kuhoji vyama vya siasa na wanasiasa Tanzania wanajifunza nini kufuatia mchakato wa uchaguzi ndani ya chama tawala cha (ANC) uliofanyika Afrika Kusini mwanzoni mwa wiki hii kumpata kiongozi wa chama hicho.
Chama tawala cha African National Congress (ANC) kilikuwa na uchaguzi wa ndani kumtafuta kiongozi wa juu ya chama hicho ambapo kulikuwa na zoezi la uchaguzi na nafasi hiyo kugombewa na wananchama wa chama hicho na kupigiwa kura, ambapo mwisho wa siku Cyril Ramaphosa aliibuka mshindi kwa kura nyingi zaidi dhidi ya Nkosazana Dlamini-Zuma hivyo Cyril Ramaphosa kutangazwa Rais wa (ANC).
"Tunajifunza nini kwa mchakato uliopelekea kupatikana kwa Cryll Ramaphosa kama Mwenyekiti wa ANC!? Alihoji Nape Nnauye
Uchaguzi wa Chama tawala nchini Afrika Kusini (ANC) ulitofautiana na uchaguzi wa Chama Tawala nchini Tanzania ambapo Mwenyekiti wake alipatikana kwa kupigiwa kura ya Ndiyo au Hapana wakati Afrika Kusini nafasi hiyo iligombewa na mtu zaidi ya mmoja.
Social Plugin