Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi Kusini mashariki ya Ziwa Victoria, Dk. Emmanuel Joseph Makala, leo Jumapili Disemba 10,2017 amezindua mnara wa maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo KKKT duniani katika Usharika wa Ebenezer Kanisa Kuu Shinyanga.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Dk. Askofu Makala amesema mnara huo ni alama iliyobeba ujumbe wa matengenezo ya kanisa ikiwa na maana wokovu wa mwanadamu unapatikana kwa NEEMA TU, NENO TU na KRISTO TU yaliyoletwa na Martine Luther katika mapinduzi ya kanisa yaliyofanyika mwaka 1517 na Martine Luther huko Ujerumani alipotundika hoja 95
Maadhimisho hayo yaliambatana na ibada ya ubarikio wa kipaimara wa watoto 107 wa Usharika huo ambapo Askofu Makala amewaasa na kuwataka watoto hao kumtumikia Mungu katika roho na kweli kwani huu ndio wakati wao wa kuanza kumtumikia Mungu.
Akizungumzia msamaha uliotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli kwa wafungwa 1828 akiwemo Babu Sega na mwanaye Papii Kocha, Askofu Makala amesema jambo hilo ndiyo maadhimisho halisi ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa kwani kilichotolewa na mheshimiwa Rais ni NEEMA TU.
Maadhimisho haya kikanisa (kitaifa) yalifanyika tarehe Oktoba 1-8 2017 jijini Arusha
Mnara wa alama ya matengenezo ya Kanisa kabla haujazinduliwa
Askofu Dk. Emmanuel Makala akizungumza na washarika juu ya mnara huo kabla ya kuuzindua rasmi
Askofu Dk. Emmanuel Makala akitoa ufafanuzi zaidi kwa washarika juu ya maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo ya Kanisa
Msaidizi wa Askofu Trafaina Nkya (wa pili kutoka kulia), Wachungaji na mashemasi wakimsikiliza askofu Makala akielezea juu ya maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa wakati wa uzinduzi wa mnara wa alama ya madhimisho hayo
Askofu Makala akizindua mnara wa alama ya maadhimisho ya matengenezo ya kanisa
Askofu Makala akizindua mnara huo
Askofu Dk Emmanuel Makala akikata utepe ikiwa ni alama ya uzinduzi wa mnara wa maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa
Askofu Dk. Emmanuel Makala akizungumza baada ya kuzindua mnara wa alama ya matengenezo ya kanisa ya miaka 500
Muonekano wa mbele wa mnara wa alama ya maadhimisho ya matengenezo ya kanisa ya miaka 500
NEEMA TU (Ujumbe mojawapo wa mnara wa alama ya maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa)
IMANI TU (Ujumbe mojawapo wa mnara wa alama ya maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa)NENO TU (Ujumbe mojawapo wa mnara wa alama ya maadhimisho ya miaka 500 ya matengenezo ya kanisa)
Picha zote na Isaac Luhende - Masengwa Blog