Wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihimiza ulipaji wa kodi wapo wahujumu uchumi na wanaotumia vibaya Sera ya Tanzania ya viwanda.
Kupitia oparesheni iliyofanyika juzi usiku, Jeshi la Polisi mkoani Mwanza limefanikiwa kubaini Kiwanda bubu cha pombe bandia kilichokuwa kinazalisha pombe kali iliyopewa jina la 'kubumba'
Polisi wamekifunga kiwanda hicho na kumkamata mmiliki wake, Emanuel George Munisi maarufu kama CCM pamoja na wenzake wanne.
Pombe hizo zilikuwa zikitumia stempu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), na meneja msaidizi wa TRA Mwanza amesema wanafuatilia kujua mtuhumiwa alipataje stempu hiyo bila kuwa na kibali
Advertisement
Social Plugin