Miili 14 ya askari wa JWTZ waliouawa nchini Kongo walikokuwa wakilinda amani, imewasili nyumbani nchini Tanzania leo na ndege ya jeshi la ya Umoja wa Mataifa, kwenye uwanja wa ndege wa jeshi jijini Dar es salaam.
Zoezi la kupokea miili hiyo limeongozwa na Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi, na maaskari wengine wa JWTZ ambao walishusha miili hiyo na kupiga gwaride mbele ya miili ya askari hao.
Baada ya miili hiyo kupokelewa uwanja wa ndege itapelekwa katika hospitali ya jeshi ya Lugalo ili kuwapa fursa maafisa kuifanyia uchunguzi miili hiyo, kabla ya kutangazwa kwa tarehe ya mazishi.
Ijumaa ya Desemba 8 Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alitoa taarifa ya vifo vya askariu hao ambao walikuwa nchini Kongo kulinda amani, huku 44 wakijeruhiwa vibaya, 8 wakiwa mahututi na wawili hawajulikani waliko.