Picha : SAVE THE CHILDREN YATOA MSAADA WA GARI,PIKIPIKI KUENDELEZA MAPAMBANO DHIDI YA UKATILI WA WATOTO KAHAMA


Shirika la Kimataifa la Save The Children limetoa msaada wa gari aina ya Toyota Landcruiser katika Halmashauri ya Mji Kahama mkoa wa Shinyanga kwa ajili ya kusaidia ufuatiliaji wa matukio ya ukatili na unyanyasaji wa watoto. 


Mbali na kukabidhi gari hilo,Save The Children pia imekabidhi pikipiki mbili aina ya Boxer,Kompyuta mpakato moja (Laptop) na Ipad moja kwa shirika la KIWOHEDE linalotekeleza mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto katika halmashauri ya Ushetu wilayani Kahama. 

Hafla fupi ya makabidhiano hayo imefanyika leo Ijumaa,Desemba Mosi,2017 katika viwanja vya Halmashauri ya Kahama Mji wilayani Kahama,mkoani Shinyanga. 

Akizungumza wakati wa kukabidhi,gari,pikipiki,laptop na Ipad, Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima alisema vifaa hivyo vitasaidia katika utendaji kazi kupambana na ukatili dhidi ya watoto. 

“Leo ni siku ya Ukimwi duniani na sisi tumeona tushiriki katika siku hii ili kuonesha kwamba ukatili ni njia mojawapo ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, Mradi wetu umeisha lakini mapambano dhidi ya ukatili kwa watoto yanaendelea, kwa hiyo tunakabidhi gari hili ili mapambano yaendelee”,alisema Malima. 

“Vifaa hivi likiwemo gari hili vitakwenda kufanya kazi za mapambano dhidi ya ukatili wa watoto,tunaomba likafanye kazi kama ilivyokusudiwa ili kuhakikisha kuwa vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vinaisha mkoani Shinyanga”,aliongeza Malima. 

Aidha alisema tangu mwaka 2014 walikuwa wanatekeleza mradi wa Ukatili dhidi ya watotokatika halmashauri ya Mji Kahama,Manispaa ya Shinyanga na Shinyanga Vijijini na baada ya mradi kuisha mwaka huu wametoa gari hilo kwa halmashauri ya Kahama Mji kwani imekuwa mstari wa mbele katika mapambano ya ukatili dhidi ya watoto. 

“Tunawapongeza sana halmashauri ya Kahama Mji kwa kuwa mfano mzuri katika vita dhidi ya ukatili wa kijinsia na watoto,wameonesha hatua za ziada,waliamua kuubeba mradi huu na kuufanya wao,tunaamini wataendeleza mapambano”,alisema Malima. 

Hata hivyo,Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Kahama Mji,Robert Kwela aliuhakikishia uongozi wa shirika hilo kuwa watalitunza na kulitumia gari hilo kwa malengo yaliyokusudiwa. 

“Mradi wa wenzetu Save the Chidren kuisha muda wake, wamekabidhi vifaa hivi ili shughuli za mapambano ya ukatili dhidi ya watoto ziendelee”,alisema. 

“Baada ya mradi kuisha,ili shughuli zilizokuwa zinatekelezwa ziweze kuendelea,utaratibu huwa ni lazima mashirika husika yaendelee kuona namna ya kujenga uwezo kwenye taasisi ambazo walikuwa wanafanya nazo kazi ili shughuli zilizokuwa zimeanzishwa ziweze kuendelezwa”,alifafanua Kwela. 

Kwa upande wake,Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija alilishukuru shirika hilo kwa ushirikiano ambao limekuwa likiwapa na kuongeza kuwa suala la ukatili dhidi ya watoto linapaswa kufanywa kwa vitendo kama vile Save the Children walivyoonesha kwa kutoa vifaa hivyo vya kutendea kazi. 

Naye Mratibu wa Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE, Lulu Makwale alilishukuru shirika la Save the Children kwa kuwapatia msaada wa pikipiki mbili,laptop na Ipad vifaa ambavyo vitasaidia katika utekelezaji wa mradi huo katika Halmashauri ya Ushetu.

Makabidhiano hayo pia yalishuhudiwa na Katibu tawala mkoa wa Shinyanga,Albert Msovela alilishukuru shirika hilo kwa msaada wa gari na kuongeza kuwa litasaidia katika kupunguza changamoto ya usafiri katika halmashauri hiyo.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO YALIYOJIRI WAKATI WA MAKABIDHIANO HAYO
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akizungumza wakati akikabidhi gari katika halmashauri ya Kahama Mji na pikipiki,laptop na Ipad kwa shirika la KIWOHEDE leo katika viwanja vya Kahama Mji,wilayani Kahama- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akizungumza wakati  wa makabidhiano hayo.Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija. Kulia ni Mratibu wa ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala shirika la Save The Children,Alex Enock akifuatiwa na Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Kahama Mji,Robert Kwela.
Gari na pikipiki zilizotolewa na shirika la Save The Chilren vikiwa nje ya ofisi za halmashauri ya Kahama Mji.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga, Benety Malima (kulia) akimkabidhi funguo za gari Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija. 
Katikati ni Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija akionesha funguo za gari lililotolewa na shirika la Save the Children kwa ajili ya kuendeleza mapambano dhidi ya ukatili wa watoto.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija akiingia kwenye gari wakati wa makabidhiano hayo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija akiwa ndani ya gari.Mwingine aliyemo ndani ya gari ni Mratibu wa mradi wa afya ya uzazi na jinsia na mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto kutoka Save the Children, John Komba (kulia).
Kulia ni Katibu tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akiwa katika eneo la makabidhiano.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama Mji,Underson Msumba ambaye awali hakuwepo wakati wa makabidhiano hayo,naye akaamua kupanda kwenye gari na kujaribu kuliendesha.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kahama Mji,Underson Msumba akiendesha gari hilo.
Kushoto ni Katibu tawala mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akimshukuru Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga, Benety Malima kwa kuipatia gari halmashauri ya Kahama Mji.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akionesha funguo za pikipiki kabla ya kukabidhi pikipiki hizo kwa Mratibu wa Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE, Lulu Makwale (kulia).
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akishikana mkono na Mratibu wa Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE, Lulu Makwale wakati wa makabidhiano hayo.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akiwa ameshikilia laptop aina ya Dell kwa ajili ya kumkabidhi Mratibu wa Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE, Lulu Makwale (kulia).
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akikabidhi laptop kwa Mratibu wa Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE, Lulu Makwale (kulia).
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima akikabidhi Ipad kwa Mratibu wa Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE, Lulu Makwale (kulia).
 Mratibu wa Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE , Lulu Makwale akionesha Ipad baada ya kukabidhiwa na Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga,Benety Malima.
Mratibu wa Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE , Lulu Makwale akionesha Ipad na funguo za pikipiki.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija akizungumza wakati wa makabidhiano hayo
Mratibu wa Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE , Lulu Makwale akizungumza wakati wa makabidhiano hayo.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija akimkabidhi Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga, Benety Malima, cheti  cha kutambua kazi nzuri zilizofanywa na shirika hilo kwenye halmashauri ya Kahama Mji hususani katika mapambano dhidi ya ukatili wa watoto.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akionesha cheti kilichotolewa na halmashauri ya Kahama Mji kutambua kazi za shirika la Save The Children.
Mratibu wa ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala shirika la Save The Children,Alex Enock  akiwa ameshikilia cheti hicho.Katikati ni Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga, Benety Malima.Kulia ni Mratibu wa mradi wa afya ya uzazi na jinsia na mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto kutoka Save the Chilren, John Komba.
Awali kabla ya makabidhiano ya  gari,pikipiki,laptop na Ipad: Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Kahama Mji, Robert Kwela akieleza namna halmashauri hiyo ilivyoshirikiana na shirika la Save the Children katika mapambano dhidi ya ukatili wa watoto.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Kahama Mji,Abel Shija akisaini fomu za makabidhiano ya gari. Aliyesimama ni Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga, Benety Malima.
Afisa Maendeleo ya Jamii,dawati la jinsia katika halmashauri ya Kahama Mji,Mary Chima akisaini fomu ya makabidhiano ya gari.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Kahama Mji, Robert Kwela akisaini fomu ya makabidhiano ya gari.
Meneja wa Shirika la Save The Children mkoa wa Shinyanga, Benety Malima akisaini fomu za makabidhiano ya pikipiki,laptop na Ipad. Aliyekaa ni Mratibu wa Mradi wa kupambana na mila na desturi kandamizi kwa watoto Shirika la KIWOHEDE , Lulu Makwale.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post