Shirika la Kimataifa la Save the Children kwa kushirikiana na shirika la Rafiki SDO la mjini Shinyanga wamefanya mkutano wa ‘Klabu za Tuseme’ kutoka shule 8 za msingi na sekondari katika manispaa ya Shinyanga na halmashauri ya Shinyanga (Vijijini) kwa ajili ya kufanya tathmini juu ya klabu hizo katika kupiga vita ukatili dhidi ya watoto.
Mkutano huo umefanyika leo Jumatano Disemba 6,2017 katika ukumbi wa Empire Hotel Mjini Shinyanga na kukutanisha wanafunzi kutoka za shule za Ushirika, Mwasele,Solwa,Bugoyi A, Lyabusalu,Masekelo, Iselamagazi na Mwantini.
Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la kuhudumia watoto la Save the Children Alex Enock, alisema Klabu za Tuseme zimeundwa kupitia mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawala unaotekelezwa na shirika la Save the Children kwa kushirikiana na Shirika la Rafiki Social Development Organization (Rafiki SDO) kwa ufadhili wa shirika la Maendeleo la nchini Sweeden (SIDA).
Enock alisema lengo la klabu hizo ni kumsaidia mtoto wa kike kukabiliana na vitendo vya ukatili dhidi ya watoto ikiwemo kupewa ujauzito na kuepuka vishawishi mbalimbali ili aweze kumaliza masomo yake salama.
Naye afisa mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawala kutoka Shirika la Rafiki SDO,Tangi Clement alisema katika kutekeleza mradi huo wameshirikiana na idara ya elimu msingi na sekondari kuanzisha Klabu za Tuseme kwa ajili ya kuhamasisha ufaulu hasa kwa watoto wa kike.
“Wanafunzi katika klabu hizi tunawajengea uelewa juu ya masuala ya haki,wajibu na ulinzi wa mtoto pamoja kutoa mafunzo elekezi kwa viongozi na walimu walezi wa klabu hizi ili kupaza sauti kukataa ukatili dhidi ya watoto”,alisema Clement.
Wakizungumza katika mkutano huo,wanafunzi hao walisema klabu hizo zimewasaidia kwa kiasi kikubwa kujiamini,kuepuka vishawishi mbalimbali lakini pia wamekuwa mabalozi wazuri katika kuielemisha jamii juu ya haki za watoto.
Mwandishi wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha za matukio yaliyojiri katika mkutano huo
Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akizungumza wakati wa mkutano wa klabu za tuseme katika ukumbi wa Empire Hotel mjini Shinyanga leo- Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akizungumza ukumbini
Afisa mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawalakutoka Shirika la Rafiki SDO,Tangi Clement akizungumza katika mkutano huo wa klabu za tuseme
Mwanafunzi kutoka shule ya msingi Ushirika akielezea namna klabu za tuseme zinavyosaidia katika kupigania haki za watoto.
Mmoja wa wanafunzi hao akielezea kazi za klabu za tuseme.
Wanafunzi wakielezea kuhusu klabu ya tuseme katika shule ya sekondari Mwantini.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Bugoyi A akielezea shughuli wanazofanya katika klabu yao ya tuseme
Mratibu wa ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akiwasilisha mada kuhusu ukatili dhidi ya watoto
Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akiendelea kuwasilisha mada ukumbini
Walimu walezi wa wanafunzi klabu za tuseme wakiwa ukumbini
Wanafunzi wakifanya kazi ya vikundi wakati wa mkutano huo
Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akiangalia wanafunzi wakifanya kazi ya kikundi chao
Afisa mradi wa ulinzi wa mtoto,haki na utawalakutoka Shirika la Rafiki SDO,Tangi Clement akiangalia wanafunzi wakifanya kazi ya kikundi
Walimu walezi nao walikuwa na kazi kwenye kundi lao. Kulia ni Mratibu wa Ulinzi wa mtoto,haki za watoto na utawala kutoka Shirika la Save The Children, Alex Enock akiwa katika kundi la walimu walezi wa wanafunzi
Washiriki katika mkutano huo wakiwa katika picha ya pamoja
Picha ya pamoja washiriki wa mkutano huo.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog