Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha : WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHA NYUZI CHA JOC SHINYANGA


Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ametembelea kiwanda cha nyuzi za pamba cha JOC Textile Tanzania Company Limited kilichopo katika kata ya Kizumbi manispaa ya Shinyanga.

Akiwa katika kiwanda hicho Mheshimiwa Majaliwa amejionea shughuli za uzalishaji nyuzi za pamba katika kiwanda hicho kinachomilikiwa na raia wa China kabla ya kukutana na wadau wa pamba kutoka mikoa 16 inayolima zao la pamba nchin.

Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametusogezea picha za matukio 
Meneja mkuu wa kiwanda JOS,Jim Liu akimuonesha Waziri Mkuu Kassim Majaliwa pamba kwa ajili ya kutengeneza pamba
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwa katika kiwanda cha nyuzi cha JOS
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia nyuzi za pamba zilizotengenezwa katika kiwanda cha JOS
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia nyuzi zinazoendelea kutengenezwa
Meneja mkuu wa kiwanda JOS,Jim Liu akiwa na Waziri Mkuu,kushoto ni mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack
Nyuzi za pamba 
Waziri mkuu Kassim Majaliwa akiangalia nyuzi za pamba
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akizungumza jambo katika kiwanda cha JOS
Awali Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasili katika uwanja wa ndege wa Ibadakuli katika manispaa ya Shinyanga
Viongozi mbalimbali wa mkoa wa Shinyanga wakimsubiri Waziri Mkuu Kassim Majaliwa 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiteremka kwenye ndege
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Zainab Telack
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiondoka katika uwanja wa ndege wa Ibadakuli kuelekea kwenye kiwanda cha nyuzi za pamba cha JOC.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com