VIJANA 84 WAHITIMU MAFUNZO YA MGAMBO KATA YA MHANGE - KAKONKO...RC NDAGALA AWAHAMASISHA KULINDA AMANI

Vijana  waliohitimu mafunzo ya jeshi la akiba katika kata ya Mhange wilayani Kakonko mkoani Kigoma wametakiwa kuyatumia mafunzo yao katika kukabiliana na vitendo vya uvunjifu wa amani katika jamii.

Rai hiyo ilitolewa jana na mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala hapo wakati akifunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Mhange ambapo jumla ya vijana 84 wamehitimu mafunzo yao.

Kanali Ndagala alisema kumekuwa na matukio mbalimbali ya kiharifu yanayotokea hasa ukilinganisha na kata hiyo kiwa karibu na nchi jirani ya Burundi hivyo ni vyema vijana hao kutumia mafunzo yao katika kuimarisha usalama ndani ya kata hiyo.

"Ningependa kuona mafunzo yenu yanakuwa chachu ya kuimarisha ulinzi na usalama kwenye maeneo yenu msiende kuwa sehemu ya waharifu na kuharibu dhima ya kuwa na mafunzo ya mgambo nitarajie kuona amani,uwajibikaji,na mambo mengine ya mafanikio yakifanyika katika maeneo yenu ili wananchi waweze kufanya shughuli zao kwa usalama na kuendelea kuinua uchumi wa Wanakakonko",alisema mkuu huyo.

Aidha aliwaomba kushirikiana na wananchi kuwaibua watu wanaokodisha mashamba kwa Warundi hali inayoweza kusababisha uharifu kuongezeaka kutokana na tabia ya baadhi ya Wananchi kushirikiana na Warundi, kwani mafunzo waliyoyapata ni kw aajili ya kulinda amani na usalama wa watanzania, na kusimamia usalama wa mali za wananchi na kuweka usalama wa wananchi.

Hata hivyo aliwaasa vijana hao kuunda vikundi vya ujasiriamali kabla ya kupata ajira kwakuwa sasa ni muda wa kufanya kazi na kufanya kazi kwa ushirikiano ilikuweza kukuza vipato vyao kwa kuungana na inapotokea kazi za ulinzi wataonwa na kupewa kipaumbele na kujitahidi kuwa waaminifu.

Awali akisoma risala mbele ya mgeni rasmi, mmoja wa wahitimu hao Sarah Katunzi alisema licha ya kufikia hatua hiyo wapo baadhi ambao walishindwa kufikia mwisho wa mafunzo yao na hii nikutokana na mwitikio mdogo kwa baadhi ya wazazi kuwazuia watoto wao wasishiriki mafunzo hayo.

Alisema mafunzo hayo yamewafanya kuwa wakakamavu na watu wanaopenda kazi na kuwaomba wazazi kuendelea kuwahimiza watoto wao ambao wapo nyumbani hawana kazi wajiunge na jeshi la akiba ili wawe wazalendo na kujijengea uwezo wa kujiajiri.

Na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog Kigoma
Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikagua gwaride wakati akifunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Mhange.
Mkuu wa wilaya ya Kakonko Kanali Hosea Ndagala akikagua gwaride akizungumza wakati akifunga mafunzo ya mgambo katika kata ya Mhange.
Picha zote na Rhoda Ezekiel - Malunde1 blog Kigoma

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post