WATOTO 1300 WALIOPOTEA KIBITI WAANZA KUPATIKANA



JESHI la Polisi mkoani Pwani limesema kuwa baadhi ya wanafunzi wa shule za sekondari na msingi, walioripotiwa kupotea mkoani humo hususani katika eneo la Kibiti, wameanza kupatikana.

Mwishoni mwa mwezi uliopita, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro alifanya ziara ya kikazi mkoani Pwani na kuagiza kufanyiwa kazi kwa madai ya kupotea kwa karibu watoto 1,300 mkoani humo ili ijulikane wamekwenda wapi.

Gazeti la Habarileo lilipotaka kujua ni kwa kiasi gani agizo la IGP limefanyiwa kazi, Kamanda wa Polisi mkoani Pwani, Jonathan Shana alisema kuwa baadhi ya watoto hao wamepatikana. Alisema waliopatikana ni wale waliokuwa watoro shuleni.

Bila kutaja idadi yao, Kamanda Shana alisema wanafunzi hao wamerudishwa kwa wazazi wao na wanaendelea na masomo. “Tunaendelea kuwatafuta wanafunzi wengine waliobaki kwa kushirikiana na maofisa elimu wa wilaya na kata. Tuliowapata walikuwa ni watoro tu shuleni na tumeshawakabidhi kwenye shule zao wanaendelea na masomo,”alieleza Kamanda Shana.

Mbali na hao waliopatikana, Kamanda Shana alisema kuwa Polisi inaendelea kufuatilia zaidi taarifa za baadhi ya watoto 1,300 waliopotea Kibiti waanza kurejea hao, kupelekwa nje ya nchi kwa mafunzo yanayodhaniwa kuwa ya kutumia silaha. Alisema mara nyingine watoto hupelekwa nje ya nchi kwa kigezo cha kupewa mafunzo ya dini, lakini baadae hubainika kujifunza mambo tofauti ikiwemo matumizi ya silaha.

IMEANDIKWA NA MATERN KAYERA - HABARILEO

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post