Mashabiki wa timu ya Stand United ‘Chama la Wana’ wamefunga mitaa mbalimbali mjini Shinyanga takribani saa nne wakifurahia kukabidhiwa basi la kisasa lenye thamani ya shilingi milioni 200 kusaidia timu hiyo lililotolewa na Kampuni ya vinywaji baridi ya Jambo Food Products inayomilikiwa na Salum Hamis maarufu ‘Jambo’.
Basi hilo aina ya Mercedes Benz lenye namba za usajili T841 DHY limekabidhiwa leo Jumanne Januari 9,2018,katika kiwanda cha Jambo Food Products na kushuhudiwa na mashabiki wa timu hiyo ambao mara baada ya zoezi la makabidhiano waliingia mtaani wakiandamana kwa magari,pikipiki na bajaji.
Akikabidhi basi hilo kwa uongozi wa timu ya Stand United,mkurugenzi wa kampuni hiyo,Salum Hamis alijigamba na kudai kuwa basi hilo ni la kisasa hakuna timu yoyote nchini inayomiliki basi kama hilo.
“Hili basi aina ya Mercedes Benz,hakuna timu yenye basi kama hili ambalo lina viti vinavyoweza kutumika kama kitanda,klabu zingine hadi zile kongwe zinatumia mabasi aina ya Youtong tu”,alisema Hamis.
“Leo nimetimiza ahadi niliyotoa ya kununua basi kwa ajili ya timu yetu,naamini litatumika kama motisha kwa wachezaji wetu ili kuhakikisha timu hii inafanya vizuri katika michezo,naahidi kuendelea kutoa misaada pale itakapohitajika kusaidia timu hii,pia naomba tushirikiane kutangaza kampuni ya Jambo Group”,aliongeza.
Nao viongozi wa timu hiyo,mwenyekiti wa Stand United,Dkt. Ellyson Maeja,nahodha wa timu Erick Muliro na Kocha mkuu wa timu hiyo Amas Nyangabo waliishukuru kampuni hiyo kwa kuwafadhili gari hilo ambalo watalitumia katika shughuli mbalimbali za kimichezo ikiwemo kusafirisha wachezaji.
Furaha ya usafiri kwa timu hiyo iliyokuwa imepotea kwa kipindi kirefu ikajionesha dhahiri pale mashabiki wake walipofanya maandamano wakipita kila mtaa kufurahia ufadhili wa basi hilo huku askari polisi wa usalama barabarani wakitanda katika kila barabara kuhakikisha maandamano hayo yanakuwa ya amani.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde alikuwepo eneo la tukio ametusogezea picha 51 za matukio yaliyojiri wakati mashabiki wa Stand United wakifurahia kupewa basi.
Basi la kisasa aina ya Mercedes Benz lenye thamani ya shilingi milioni 200 kusaidia timu hiyo lililotolewa na Kampuni ya vinywaji baridi ya Jambo Food Products Ltd likiwa limepaki katika kiwanda cha Jambo leo Januari 9,2018 kabla ya kukabidhiwa kwa uongozi wa Stand United-Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Mashabiki wa timu ya Stand United wakishangilia baada ya kuona basi hilo
Mashabiki wa Stand Unites wakifurahia...
Wachezaji na viongozi wa Stand United wakijiandaa kukabidhiwa basi
Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo Food Products,Salum Hamis 'Jambo' akizungumza wakati wa kukabidhi basi aina ya Mercedes Benz lenye thamani ya shilingi milioni 200 kwa timu ya Stand United
Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo Food Products,Salum Hamis akizungumza wakati wa kukabidhi basi hilo
Mashabiki wa Stand United wakimsikiliza Salum Hamis
Mwenyekiti wa Stand United,Dkt. Ellyson Maeja akizungumza wakati wa kukabidhiwa basi
Kocha wa Stand United Amas Nyangabo akizungumza wakati wa makabidhiano hayo
Nahodha wa timu ya Stand United Erick Muliro akiishukuru Kampuni ya Jambo Food Products
Mkurugenzi wa kampuni ya Jambo Food Products,Salum Hamis 'Salum Mbuzi' akimkabidhi funguo ya basi hilo nahodha wa timu ya Stand United Erick Muliro
Wachezaji wa timu ya Stand United wakipanda kwenye basi hilo
Wachezaji wa timu ya Stand United wakiwa ndani ya basi hilo
Wachezaji wa Stand united wakiwa wamekaa ndani ya basi
Dereva wa Stand United Tungu Mathias akijiandaa kuendesha basi hilo
MAANDAMANO BAADA YA MAKABIDHIANO YA BASI: Mashabiki wa Stand United wakiondoka katika kiwanda cha Jambo
Hapa ni katika eneo la Ibadakuli,barabara ya Shinyanga - Mwanza Mashabiki wa timu ya Stand United wakiandamana kuelekea Shinyanga Mjini
Maandamano yanaendelea katika barabara ya Shinyanga - Mwanza
Msafara wa mashabiki wa Stand United wakiandamana kufurahia basi
Hapa ni katika Daraja la Mhumbu...
Msafara ukiingia katika Stendi ya Mabasi yaendayo wilayani
Mashabiki wa Stand United wakiwa katika Stendi ya Mabasi yaendayo wilayani 'Stendi ya Zamani' mjini Shinyanga
Misafara ya magari ya waandamanaji ikiwa katika Stendi ya mabasi yaendayo wilayani
Magari yakiingia katika Stendi ya mabasi yaendayo wilayani
Basi la kisasa aina ya Mercedes Benz likitoka katika Stand ya Mabasi yaendayo katika wilaya mbalimbali 'Stand ya Zamani' ambako ndiko timu hiyo ilianzia
Hapa ni katika eneo la barabara ya Shinyanga- Old Shinyanga maandamano yakiendelea
Maandamano yakiendelea ...mjini Shinyanga
Eneo la Mnara wa Voda pia maandamano yalipita
Maandamano yanaendelea...
Eneo la Uhuru Sekondari...
Maandamano yanaendelea
Barabara jirani na Stendi ya mabasi iliyopo eneo la Soko Kuu Mjini Shinyanga
Hapa jirani na Benki ya NMB Manonga
Eneo la Phantom ..
Daraja la Ibinzamata...
Askari polisi wakiendelea kuongoza maandamano
Mashabiki wa Stand United wakiingia katika Stendi ya Mabasi yaendayo Mikoani maarufu 'Manyoni'
Waandamanaji wakiwa katika Stend ya mabasi yaendayo mikoani
Wanafunzi wa shule ya Msingi Ibinzamata wakishangaa waandamanaji...
Eneo jirani na Machinjio ya mbuzi Ibinzamata..
Eneo la Phatom
Jirani na gesti ya Rwezahula
Hapa ni jirani na Soko na Nguzo Nane
Jirani na ofisi za shirika la AGPAHI,Kambarage
Barabara ya Kambarage kuelekea Janapanese Kona
Eneo la round about,Japanese kona
Eneo jirani na mahakama kuu
Hapa ni katika Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga
Kondakta wa basi la Mwanza Express na abiria wakishangilia wakati mashabiki wa Stand United wakiandamana
Hapa ni katika eneo la Kalogo,relini maandamano yakiendelea.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin