Fedha zilizotengwa na Rais John Magufuli kwa ajili ya kugharimia elimu bure nchini, zimeanza kutafunwa baada ya kubaini kuwapo kwa udanganyifu, unaofanywa na walimu wakuu wilayani Kalambo katika Mkoa wa Rukwa.
Taarifa zinaeleza kuwa baadhi ya walimu wakuu wilayani Kalambo, wanadaiwa kuzifanyia u.
badhirifu fedha hizo, kwa mbinu ya kufanya udanganyifu wakati wa ununuzi wa vitabu na karatasi kila mwezi zinapotolewa fedha hizo.
Kufuatia udanganyifu huo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kalambo, Daud Sichone amemwagiza Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Simon Ngagani kutuma mara moja wakaguzi wa ndani, kukagua hesabu katika shule zote za msingi na sekondari za umma wilayani humo ili kujiridhisha na matumizi ya fedha hizo.
Alitoa agizo hilo alipokuwa akizungumza na madiwani wa halmashauri hiyo wakati akifungua kikao maalumu cha Bajeti, kilichokaa katika mji mdogo wa Matai juzi.
“Nimefanya ziara hivi karibuni ya kutembelea shule za msingi zilizopo katika kata yangu ya Kitete na nilibaini kuwa fedha hizo hazitumiki kama ilivyokusudiwa baadala yake walimu wakuu wamebuni mbinu ya kuzitafuna kwa kila mwezi kuzinunulia vitabu na makatarasi.
Na Pety Siyame- Habarileo Kalambo
Social Plugin