KATIBU MKUU WA CHADEMA DK MASHINJI ADAI NI MZIMA...WAPUUZWE WANAOSEMA KAUGUA GHAFLA
Thursday, January 18, 2018
Katibu Mkuu wa Chadema, Dkt. Vincent Mashinji amesema yeye ni mzima na huenda kuna makosa yametokea kumuhusisha yeye kuwa ni mgonjwa.
Muda mfupi baada ya kuripotiwa kuwa ameugua ghafla na kupelekwa Hospitali ya Amana,Dkt Mashinji amesema kuwa yeye ni mzima na anakula ugali. Hivi sasa yuko katika kikao cha Kamati Kuu ya Chadema inayoendelea jijini Dar es Salaam.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin