Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUHUSU BALAA LA WANAOUZA MIILI YAO,WAVAA MILEGEZO NA WAPENDA UCHI DAR

Jeshi la Polisi Kanda Maalum jijini Dar es salaam linaendesha oparation maalumu ya kuwakamata watu wanaofanya biashara ya kuuza mwili, pamoja na wale wanaowahifadhi kwenye nyumba zao.

Taarifa hiyo imetolewa jana na Kamanda Lazaro Mambosasa ambapo amesema kufanya hivyo ni kosa kisheria na uvunjifu wa maadili hivyo ni lazima wachukuliwe hatua, pamoja na wale wanaovaa mavazi yasiyostahili kwa eneo husika.

“Kuvaa nguo fupi ni kosa la kimaadili, na sisi tunapofanya misako tunaangalia ni kosa gani limekiukwa kutokana na sheria za nchi, misako tunayoifanya tunalenga watu wanaoishi kwa kujiuza na kujipatia mapato, lakini kuvaa nguo fupi mwengine ni utamaduni wake, kwenye fukwe ukikutwa umevaaa suti tutakushangaa, lakini mtu huyo wa fukwe tukimkuta kanisani, tukimkuta msikitini tutamkamata tu”, amesema Mambosasa

Operation hiyo ya jeshi la polisi kukamata watu haitakuwa mara ya kwanza, kwani ilishawahi kufanyika siku za nyuma na kukamata baadhi ya watu wanaojihusisha na biashara hiyo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com