Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUNGURU AZUIA NDEGE YA WANAJESHI KUPAA ANGANI


Picha ya Kunguru

Kunguru mmoja amelazimu ndege iliyokuwa imewabeba wanajeshi wa Amisom kutoka Burundi kutua kwa ghafla katika uwanja wa ndege wa Bujumbura nchini Burundi. 

Ndege hiyo inadaiwa kumgonga kunguru huyo angani wakati ilipokuwa ikipaa , kabla ya rubani kuamua kutoendelea na safari ya kuelekea Somalia ambapo wanajeshi hao wanahudumu kulingana na vyanzo vya habari na wizara ya ulinzi katika uwanja huo. 

Ndege hiyo ilisalia hewani kwa takriban saa moja kabla ya kutua.

Afisa mkuu wa uwanja wa ndege wa Burundi Emmanuel Habimana amethibitisha kuwa ndege hiyo iligonga kunguru huyo mapema alfajiri. 

Hata hivyo kulingana na afisa huyo hakukuwepo na tatizo lolote la kiufundi na ndege hiyo iliondoka tena. 
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza ametangaza kuwa serikali yake inajiandaa kuishtaki EU 

Wanajeshi wa Burundi ni miongoni mwa wanajeshi wa Umoja wa Afrika wanaokabiliana na wapiganaji wa Al-Shabab nchini Somalia.
Wanajeshi wa BurundiWanajeshi wa AU nchini Somalia 

Chanzo-BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com