Toka Mwaka jana mwezi wa 12 baada ya mimi kupiga picha katika mojawapo ya Hostel za Dr. John Pombe Magufuli iliyokuwa ikionyesha nyufa kumekuwa na watu ambao wamekuwa wakinifuatilia mara kwa mara kila mahali ninapoenda, (Siwezi kusema kupiga picha za nyufa ndio sababu ya kunifuatilia kwangu au la), awali nilidhani labda wanashughuli zao lakini kilichonishangaza ni kuwa kila siku zinavyoidi kwenda nikikaa sehemu watu hawa nao walikuwa wanakaa umbali kidogo nilipo mimi, nami nikianza kuondoka nikigeuka nyumba nabaini kuwa wananifuatilia.... Siku zinavyozidi kwenda nimebaini watu wale walikuwa na nia mbaya kwangu.
Wiki jana, siku ya Alhamisi nikiwa natoka Mlimani City nilianza kutembea kurudi zangu hosteli nikipita ile njia ya Service road mbele yangu niliona gari aina ya Noah imepaki na mlango ukiwa wazi (Mbele kidogo ya geti la Mlimani City) nilivyofika kwenye ile gari watu wale walinitaka niingie kwenye gari huku wakiwa ndani ya gari lile! Mimi niliwajibu, "Mnanifahamu??.... Mnajua ninakoenda??...... Wakati nikiwauliza haya maswali walianza kushuka kwenye gari huku wakiniambia sio lazima kutujua sisi ni akina nani...... " Ingia kwenye gari haraka" waliniambia kwa ukali.
Namshukuru Mungu kulikuwa na watu jirani wakiwemo wakiwemo waendesha bajaji waliokuwa wamepaki nyuma kidogo, hivyo nilipiga kelele kuwaeleza kuwa wanataka kuniteka.
Baada ya mimi kupiga kelele watu wale waliokuwa wanashuka kunitaka kunilazimisha niingie kwenye gari waliingia haraka na kuliondosha gari lile.... Kipekee niwashukuru waendesha bajaji kwa msaada wenu, hakika msingekuwepo nyinyi pale leo tungekuwa tunazungumza mengine.
Baada ya tukio lile niliripoti kwenye vyombo tofauti vya ulinzi ikiwa ni pamoja na Polisi wasaidizi (Auxiliary Police) na Polisi wenyewe na kuandikiwa RB yenye kumbukumbu namba UD /RB/344/2018...... Polisi waliniomba endapo nitaziona sura zile mahali popote zikinifuatilia nitoe taarifa huku wakiniomba nisitembee peke yangu kila sehemu ninapoenda na kunieleza kuwa nitakapoona inafaa nijilinde.
Hali kadhalika suala hili niliripoti kwa walezi wangu wanaonilea kwa maana ya Ofisi ya Mshauri wa Wanafunzi hapa chuoni kwangu.
Rai yangu kwa nyie vipele mnaonifuatilia waambieni hao wanao watuma wauache utoto....... Mlimpa nini Kumbusho Dawson mpaka mnamfatilia hivi??? kama mnanidai njooni nitawalipa.
Shame be upon you!!!!
Shubamitiiiiiiiiii.
Shubamitiiiiiiiiii.
Social Plugin