Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini Chadema Mchungaji Peter Msigwa amesema mbinu inayotumika kuwashawishi na kuwanunua madiwani wa Chama hicho imelenga kupunguza nguvu zake katika kuikosoa Serikali.
Amesema taarifa hizo amepewa na viongozi wa CCM ambao wamemthibitishia kuwa hawana shida nao.
"CCM hawana shida na madiwani, wanachama wanashida na wale wakosoaji wakubwa wa Serikali Kuu"amesema Msigwa
Msigwa amewataja wabunge wengine wa upinzani aliodai watapitia kipindi hicho kuwa ni Mbunge wa Jimbo la Hai Freeman Mbowe, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki Tundu Lisu, Mbunge wa Jimbo la Mbeya Joseph Mbilinyi, Mbunge wa Kawe Halima Mdee na Mbunge wa Arusha Mjini Godbles Lema.
Social Plugin