Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Kangi Lugola amefiwa na mkewe Mary.
Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais imesema Mary amefariki dunia leo Jumatatu Januari Mosi, 2018 jijini Dar es Salaam.
Wakati huohuo, Ofisi ya Bunge katika taarifa kwa umma imesema Spika Job Ndugai amemtumia rambirambi Lugola kutokana na kifo cha mkewe.
Imeelezwa msiba upo Railway Club Gerezani jijini Dar es Salaam.
Ndugai ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki kwa kumpoteza mpendwa wao.
Social Plugin