Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

NYUMBA YA KIONGOZI WA CCM YACHOMWA MOTO

Watu wasiojulikana wamedaiwa kuchoma moto nyumba ya Katibu wa Umoja wa Vijana Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Iringa, Alphonce Muyinga iliyopo maeneo ya Kihesa njiapanda ya Kwabeda usiku wa kuamkia leo.

Kwa mujibu wa taarifa kikosi cha Zima Moto kilifanikiwa kufika katika nyumba hiyo na kujaribu kuzima moto huo ambao tayari ulikuwa umeshaleta athari ndani ya nyumba hiyo kwa mali mbalimbali zilizokuwepo ndani. 

Mbali na hilo aliyekuwa Diwani wa kata ya Mwangata, Iringa kwa tiketi ya CHADEMA na baadaye kujiuzulu nafasi yake hiyo, Anjelus Mbogo naye amefanyiwa uharibifu katika nyumba ambayo alikuwa akijenga baada ya watu wasiojulikana kuibomoa nyumba hiyo. 

"Kauli ya Mbunge ndiyo inaweza kuwa chanzo cha uchochezi kwa wananchi kuja kubomoa nyumba hizi kwa sababu yeye aliwaambia wananchi kama atajiuzulu wabomoe nyumba yake hata gari yake ichomwe moto nadhani wananchi wakachukua hilo kwani wananchi unapowashawishi ndivyo unavyomuaminisha kuja kufanya hivi huo ndiyo ukweli. Na mimi sisemi mambo mengi kwa kuwa jambo hilo bado linaendelea na upelelezi lakini naamini wameniaminisha kuwa hatabaki mtu" alisema Anjelus Mbogo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com