Picha : DC SHINYANGA AUNGANA NA WANANCHI KUZUIA MAJI YA BWAWA LA MWALUKWA YASITOROKE

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro leo Ijumaa Januari 26,2018 ameungana na wananchi wa kijiji na kata ya Mwalukwa iliyopo katika halmashauri ya wilaya ya Shinyanga (Vijijini) kuziba ukingo wa bwawa la Mwalukwa ambao umebomoka na kusababisha maji yatoroke.


Matiro aliyekuwa ameambatana na mkurugenzi wa halmashauri hiyo Bakari Kasinyo Mohamed pamoja na baadhi watendaji wa halmashauri akiwemo Injinia wa maji Silvester Mpemba aliungana na wananchi kuziba sehemu ya ukuta/ukingo wa bwawa iliyobomoka na kusababisha maji yavuje/yatoroke.

Bwawa hilo lililojengwa kwa nguvu ya wananchi kati ya mwaka 1948- 1951 linahudumia wananchi wa kata ya Mwalukwa yenye vijiji vinne ambavyo ni Ng’hama,Bulambila,Mwalukwa na Kadoto B lakini pia kijiji cha Mwamadilanha kilichopo katika kata ya Pandagichiza.

Akizungumza wa zoezi hilo la kuziba sehemu ya bwawa inayovuja,Mkuu wa wilaya ya Shinyanga,Josephine Matiro aliwataka wananchi kutunza bwawa hilo wakati serikali inaendelea na utaratibu wa kufikisha huduma ya maji ya mradi wa Ziwa Victoria katika vijiji ambavyo havijafikiwa na mradi huo.

“Nimekuja hapa kuungana nanyi kuongeza nguvu ya kuzuia maji yasitoke,niwapongeze pia kwa kuja,naomba mtunze bwawa hili kwani kuna maeneo mengine wanatamani kuwa na bwawa kama hili,maafisa watendaji ,viongozi wa sungusungu na viongozi ngazi za vijiji na kata wekeni utaratibu wa kutunza hili bwawa kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo yenu”,alisema Matiro.

Hata hivyo Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga,Bakari Kasinyo Mohamed alisema pesa zilizotengwa kwa ajili ya ujenzi wa bwawa hilo bado hazijafika hivyo kuwataka wananchi kutokuwa na hofu kuwa huenda pesa zimeliwa na baadhi ya watu.

Nao Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela na katibu wake Jumanne Katundu walioshiriki katika zoezi hilo,waliwaomba viongozi wa vijiji na kata kuunda sheria na kanuni kwa ajili ya kutunza bwawa hilo.


ANGALIA VIDEO JINSI UKUTA WA BWAWA ULIVYOBOMOKA
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (wa tatu kushoto) akiangalia maji yaliyotoroka katika bwawa la Mwalukwa lililopo katika kata ya Mwalukwa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga.Kulia ni wananchi wa kijiji cha Mwalukwa wakiweka mchanga kwenye mifuko ili kuzuia maji yasitoroke katika bwawa hilo. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwa ameshikilia jembe tayari kuanza kushirikiana na wananchi kuweka mchanga katika eneo ambalo maji yametoroka. Wa pili kushoto ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Jumanne Katundu.
Sehemu ya bwawa la Mwalukwa.
Kulia ni diwani wa kata ya Mwalukwa Ngassa Mboje akionesha sehemu ambayo bwawa limemong'onyoka ukuta na kusababisha maji yavuje/yatoroke.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akifukia sehemu ya ukingo wa bwawa hilo.
Muonekano wa sehemu ya bwawa hilo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) akishirikiana na wananchi wa kijiji cha Mwalukwa kuchimba udongo kwa ajili kuziba sehemu ya ukuta/ukingo uliobomoka katika bwawa la Mwalukwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro (kulia) akiwa amebeba karai la udongo aliouchimba kwa ajili ya kuziba ukingo/ukuta wa bwawa la Mwalukwa.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akishirikiana na mwananchi kubeba mfuko wa udongo kwa ajili ya kuziba ukuta wa bwawa la Mwalukwa.
Akina mama wakiwa wamebeba udongo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,mwananchi na mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga  Bakari Kasinyo Mohamed (wa kwanza kulia) wakishindilia udongo kwenye sehemu ya ukingo wa bwawa uliomong'onyoka.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga  Bakari Kasinyo Mohamed akiwa ameshikilia karai.
Injinia wa maji halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Silvester Mpemba akizungumza baada ya wananchi kwa kushirikiana na mkuu wa wilaya na viongozi wa CCM kufanikiwa kuziba sehemu ya ukingo wa bwawa uliobomoka na kuwasihi kuendelea kujaza udongo katika eneo hilo kwani hiyo siyo kazi ya siku moja tu.
Kulia ni Afisa tawala wilaya ya Shinyanga, Charles Maugira akimkaribisha mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro azungumze na wananchi walioshiriki zoezi la kuziba sehemu ya ukuta wa bwawa la Mwalukwa iliyobomoka.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwasititiza wananchi kulinda bwawa hilo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro akiwataka wananchi kujitolea katika mambo ya maendeleo. 
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Jumanne Katundu akiwaomba wananchi kutunza bwawa hilo wakati serikali inafanya utaratibu wa kufikisha maji ya ziwa Victoria.Kushoto kwake ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Vijijini Edward Ngelela
Diwani wa kata ya Mwalukwa Ngassa Mboje ambaye pia ni mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga akiwashukuru wananchi kujitolea kuziba sehemu ya ukuta wa bwawa la Mwalukwa.
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Bahati Kasinyo Mohammed akiwataka wananchi kuwa wavumilivu wakati serikali inafanya jitihada za kuleta pesa kwa ajili ya ukarabati wa bwawa la Mwalukwa ambao limejaa matope na kingo zake siyo imara.
Picha zote na Kadama  Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post