Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHUWASA,KUWASA ZATANGAZA UPUNGUFU WA MAJI MJINI SHINYANGA NA KAHAMA TANESCO KUKATA UMEME



Mji wa Shinyanga na Kahama umekumbwa na tatizo la upungufu wa maji baada ya Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kukata umeme katika chanzo kikuu cha maji ya Ziwa Victoria kilichopo Ihelele wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza.

Kufuatia tatizo hilo Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Shinyanga (SHUWASA) amewatangazia wananchi wote kuwa kutakuwa na upungufu mkubwa wa huduma ya maji safi katika mji wa Shinyanga kutokana na kusitishwa kwa huduma ya umeme katika kituo cha uzalishaji maji ya ziwa Victoria kilichopo Ihelele.

Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira mjini Kahama (KUWASA) nayo imewatangazia wateja wake kuhusu upungufu wa maji katika mji wa Kahama.



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com