Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May
Uingereza imemchagua waziri wa upweke ili kukabiliana na kile ambacho waziri mkuu wa Uingereza amedai ni uhalisia wa masikitiko kuhusu maisha ya sasa yanayoathiri mamilioni ya watu.
Tracey Crouch, ambaye ni naibu waziri wa michezo na wanaharakati atachukua wadhfa huo ikiwa ni miongoni mwa malengo ya kukabiliana na upweke unaowakabili watu wazima, wale waliopoteza wapendwa wao, wale wasio na watu wa kuzungumza nao ama hata kugawana fikra na uzoefu, waziri huyo aliongezea.
Zaidi ya watu milioni tisa wanasema kuwa huwa pweke kati ya milioni 65.6 kulingana na shirika la msalaba mwekundu.
Shirika hilo limetaja upweke na kutengwa kuwa janga lililojificha miongoni mwa watu wenye miaka tofauti katika maisha yao kama vile waliostaafu , waliofiliwa ama waliotengwa.
Uanzilishi wa wizara hiyo unafuatia mapendekezo kutoka kwa kamati ya kumbukumbu za Jo Cox , mbunge wa chama cha upinzani cha leba ambaye aliuawa na watu wenye itikadi kali wa mrengo wa kulia.
Jo alikuwa na alishuhudia upweke katika kipindi chote cha maisha yake akiwa mwanafunzi mpya katika chuo kikuu cha cambridge na alijitenga na dadake Kim, kwa mara ya kwanza , wakfu wa Jo Cox uliandika katika mtandao wa twitter.
Angefurahishwa na kazi mpya ya Tracey Crouch kama waziri wa upweke na angesema twende kazi, wakfu huo uliongezea.
Chanzo- BBC
Social Plugin