Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WALIMU WAFUKUZWA KAZI KWA MICHANGO SHULENI

Halmshauri ya wilaya ya Magu mkoani Mwanza imewasimamisha kazi walimu watatu wa shule ya msingi Nenge akiwemo Mwalimu Mkuu na Afisa Elimu Kata ya Nyanguge kwa kosa la kukaidi agizo la Rais Magufuli la kutochangisha fedha wanafunzi.

Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Magu Lutengano Mwalwiba, amesema kuwa baada ya agizo la Rais Magufuli la kusitisha michango katika shule za msingi, Januari 23 mwaka huu aliwaonya wakuu wa shule na walimu wote, lakini Januari 24 waliendeleza kukusanya michango.

Mwalwiba ameongeza kuwa watumishi hao wamekiuka mkataba wa elimu ya msingi bila malipo ambapo wamewachangisha shilingi 500 wanafunzi 378 wa shule hiyo kwa ajili ya lebo zautambulisho wa sare za wanafunzi kinyume na maagizo ya Rais Magufuli. 

January 17 mwaka huu Rais John Pombe Magufuli alipiga marufuku michango kwenye shule za msingi na sekondari za serikali, na kuwaagiza Mawaziri Joyce Ndalichako na Waziri wa TAMISEMI Suleiman Jafo kusimamia agizo hilo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com