Chakula kitamu lakini kinachowaua watu Japan
Watu wawili wamefariki nchini Japan huku wengine wakiwa katika hali mbaya baada ya kusakamwa na chakula cha kitamaduni maarufu kama (mochi) ambacho ni keki zilizopikwa kutokana na mchele, wakati wa sherehe za kuukaribisha mwaka.
Chakula hicho kinaonekana kutokuwa na madhara yoyote , lakini kila mwaka kimewaua watu kadha, na kusababisha onyo kutolewa kwa umma.
Mochi ni chakula gani?
Keki zinazoitwa mochi ni nzuri zinazopikwa kutokana na mchele.
Kwanza kabisa mchele huchemshwa na kisha kupondwa na kukorogwa.
Kile kitokanacho na kupondwa kwa mchele hufinyangwa na kisha kuokwa au kuchemshwa.
Huua kwa njia gani?
Keki za mochi hunata. Kutokana na ukubwa wake zinahitaji kutafunwa sana kabala ya kumezwa.
Yeyote ambaye hawezi kukitafuna kwa njia inayostahili kwa mfano watoto au watu wazee hupata keki hizo vigumu kula.Kile kitokanacho na kupondwa kwa mchele hufinyangwa na kisha kuokwa au kuchemshwa.
Ikiwa keki hizo haziwezi kutafunwa vizuri zinaweza kukwama kwenye koo na hata kusababisha kifo.
Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Japan asilimia 90 ya wale waliokimbizwa hospitalini wakati wa sherehe za mwaka mpya walikuwa ni watu walio na miaka 65 na zaidi.
Ni njia ipi salama ya kula chakula hicho?
Tafuna, Tafuna, Tafuna. Kama hilo haliwezekani keki hizo zinastahili kukatwa vibande vidogo.
Kila mwaka mamlaka huwanonya watu hasa wazee na watoto kula mochi zikiwa zimekatwa vibande vidogo.
Licha ya onyo hilo kutolewa, kila mwaka hutokea vifo vinavyosababishwa na chakula hicho.
Social Plugin