Mwili wa mwanasiasa mkongwe Kingunge Ngombale Mwiru utaagwa katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam baada ya ibada itakayofanyika nyumbani kwake Kijitonyama.
Akizungumza jana Februari 3,2018 mtoto wa mwanasiasa huyo aliyefariki dunia katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jana Februari 2,2018, Kinje Ngombale Mwiru amesema uamuzi huo umetolewa baada ya kufanyika kikao cha familia.
“Itafanyika ibada ya Kanisa Katoliki nyumbani Jumatatu kisha tutaelekea viwanja vya Karimjee kwa ajili ya kutoa heshima za mwisho na baada ya hapo tutaeleka makaburini Kinondoni,” amesema.
Social Plugin