MKIKITA WAFURAHIA HUDUMA NZURI SPICE HOTEL LIMITED DAR


Viongozi wa Mtandao wa Kijani kibichi Tanzania (Mkikita), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Kissui Steven Kissui (Kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa mtandao huo, Adam Ngamange (wa nne kushoto), wakiwa nje ya Spice Hotel Limited, baada ya kufanya mkutano na waandishi wa habari hoteni hapo, Dar es Salaam jana.PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA
 ****

Uongozi wa Mkikita umefurahishwa na huduma za hoteli hiyo iliyopo makutano ya mitaa ya Narung'ombe na Lumumba Karikaoo Dar es Salaam na kuahidi mikutano mingine ijayo kuendelea kufanyia hapo.

Baada ya kumaliza mkutano, uongozi wa Mtandao huo ulimtembelea Mmiliki wa Hoteli Ofisi kwake, Bw. Mwangaba kwa lengo la kufahamiana pamoja na kumpa pongezi kutokana na hoteli hiyo kuwapatia huduma nzuri.

Mwangaba mwenye hoteli hiyo ya kisasa yenye vyumba 67 vyenye hadhi tofauti alishukuru na kuwakaribisha tena kwenda hapo kwa shughuli mbalimbali. Pia alikubali kujiunga na mtandao ili awe anashiriki kwenye shughuli mbalimbali zinazofanywa na mtandao huo na kunufaika nazo pia. Kwa habari zaidi kuhusu hoteli hiyo soma maelezo yaliyopo mwisho wa ukurasa huu.
Hoteli yenyewe
Viongozi wa Mkikita wakiwa katika picha ya pamoja na Mmiliki wa Hoteli ya Spice, Mwangaba (wa pili kushoto). Kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi, Dk. Kissui S. Kissui, Meneja wa Mashamba, Catherina, Ofisa wa Logistic, Morris Mwita, CEO Adam Ngamange, Ofisa Uhusiano, Neema Fredrick na Meneja Masoko, Deo.
CEO Adam Ngamange akizungumza katika mkutano na wanahabari, kuhusu maandalizi ya mafunzo ya kilimo biashara cha Papai Salama kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Hope For All, Askofu Edger Mwamfupe akizungumza kuhusu makubaliano ya ushirikiano waliosaini na Mkikita kwa lengo la kuwakomboa wananchi masikini Tanzania.
Mfanyabiashara Adamjee akielezea jinsi anavyokiendesha kwa faida kubwa kilimo cha pilipili kichaa
Mwenyekiti wa Bodi ya Mkikita, Dk. Kissui akizungumza katika mkutano huo, kuhusu kazi mbalimbali zinazofanywa na mtandao huo.
Ofisa Uhusiano wa Mkikita, Neema, akielezea utaratibu unaotumika kuwasajili watu wanaotaka kuhudhuria mafunzo ya kilimo kibiashara cha Papai Salama
Mmiliki wa Spice Hotel, Mwangaba (kulia), akizungumza alipokutana na viongozi wa Mkikita kwa lengo la kufahamiana
Mwangaba akiagana na Adam Ngamange
Mwangaba akiagana na Catherina
Mwangaba akiagana na Dk. Kissui

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post