Mwanaume mmoja ambaye alijibadilisha jinsia na kuwa mwanamke nchini Marekani, ameweza kunyonyesha mtoto kwa maziwa yake, na kuweka rekodi ya mtu kuwahi kufanya hivyo duniani. Kwa mujibu wa watafiti.
Mwanamke huyo kwa sasa mwenye umri wa miaka 30 aliamua kufanya hivyo baada ya mpenzi wake kukataa kunyonyesha mtoto waliyekuwa wakitarajia kumpata.
Mtu huyo ambaye sasa ni mwanamke aliweza kufanya hivyo baada ya kutumia dawa na mashine ya ku-'pump' maziwa, huku watafiti wakisema matokeo ya tukio hilo yanaweza yakasababisha watu wengi waliobadili jinsia kutaka kufanya hivyo.
Taarifa zinasema kwamba mwanamke huyo alikuwa akipata tiba ya kubadilishiwa homoni kwa muda wa miaka 6, na hakuwahi kufanya upasuaji wa kubadili jinsia wakati amewafuata madaktarai kuwaelezea mpango wake wa kutaka kunyonyesha.
Kabla mtoto huyo hajazaliwa madaktari walimpa mafunzo maalum ya tiba kkumsaidia kutengeneza maziwa feki, ambayo mara nyingi hupewa kina mama ambao wameasili mtoto au wamepata mtoto kwa njia ya 'Surrogate', ikiwemo kupump maziwa, kuwekewa homoni za mama asili wa mtoto, na dawa amabzo zinasisimua uzalishaji wa maziwa na kuzuia homoni za kiume
Social Plugin