Sio filamu wala maigizo, hii ni kweli tupu, fahamu historia ya binti wa Kifaransa aliyekulia msituni na wanyama na kucheza nao kama anavyocheza na binadamu bila kumdhuru, mpaka akaanza ku-adopt tabia zao.
Anafahamika kwa jina la Tippi Benjamine Okanti Degré alizaliwa tarehe 4 Juni 1990, huko Windhoek Namibia, akiwa ni mtoto wa pekee wa mpiga picha za wanyama na mtengeneza filamu wa Kifaransa, Sylvie Robert na Alain Degre.
Katika utoto wake Tippi alikulia katika nchi ya Namibia kwenye mbuga za wanyama na watu wa kabila la Bushman, ambako wazazi wake walikuwa wakifanya kazi ya kupiga picha na kutengeneza documentary za maisha ya wanyama, kitendo ambacho kilimfanya kuwa karibu na wanyama kwa kuwa hakuwa na watu wa kucheza ano.
Maisha ya Tippi yalikuwa ya kuzungukwa na wanyama wanaojulikana kwa ukali na kutokuwa na urafiki na binadamu, wakiwemo simba, chui, mamba, nyoka, tembo, na kila mnyama mabaye unajua anapatikana kwenye mbuga za Afrika.
Kwenye miaka 10 ya utoto wake Tippi aliweza kuishi na wanyama hao huku akicheza nao bila kuogopa na bila kumdhuru, huku wengine akiwapatia majina anayoyajua mwenyewe na wengine kuwaita kaka zake, na wazazi wake kushoot video za mtoto wao huyo na baadaye kutengenezea makala, ambayo watu wengi waliipenda na kurushwa kwenye baadhi ya chaneli zinazoonyesha maisha ya wanyama.
Tippi alisoma nchini Ufaransa ambako ndio nyumbani kwa wazazi wake, na mara kwa mara kwenda nchi ya Namibia ambayo ipo kusini mwa Afrika, kutokana na mapenzi aliyonayo kwa eneo hilo.
Hivi sasa Tippi ana miaka 27 na amesomea masuala ya filamu kama wazazi wake, na yuko nchini Ufaransa akifanya kazi ya kudirect filamu.
Tazama video yake hapa chini ikimuonyesha alivyokuwa akicheza na wanyama ambao ni tishio kwa binadamu.