Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Shinyanga Mjini kimefanya kongamano kuadhimisha sherehe za kutimiza miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama hicho.
Kongamano hilo lililohusu sera za CCM,Ujamaa na Kujitegemea limefanyika leo Jumamosi Februari 3,2018 katika ukumbi wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini ambapo mgeni rasmi alikuwa mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge.
Mamia ya watu wamehudhuria kongamano wakiwemo wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya,wajumbe wa halmashauri ya CCM kata za tarafa ya Shinyanga Mjini.
Wengine ni kamati za utekelezaji za mabaraza ya Jumuiya za Chama (UVCCM,UWT,Wazazi) wa ngazi za wilaya,makada,waasisi na wazee wa CCM,wakuu wa taasisi,wanafunzi wa vyuo na shule za sekondari pamoja na wanachama wa chama hicho.
Awali akizungumza katika kongamano hilo,Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Gulam Hafeez Mukadam alisema wanaCCM wana kila la kujivunia katika kusherekea miaka 41 tangu kuanzishwa kwake ambapo amani ya nchi imeendelea kudumishwa.
Gulam alitumia fursa hiyo kuwataka wanaCCM kuacha makundi kwani hakuna aliye juu ya chama hivyo ni vyema wakashirikiana katika kujenga chama na kuwaletea maendeleo wananchi.
“Ni aibu sana kwa wanachama kusemana mambo mabaya mtaani,kama kuna tatizo ni vyema tukatumia vikao vyetu kujadili yanayotuhusu badala ya kwenda kusemana mtaani,jambo hili sitaki kuliona sitakuwa tayari kuona makundi ndani ya chama”,alieleza Gulam.
Katika hatua nyingine aliwataka wanachama wa CCM kuhakikisha wanawajibika kujenga chama kwa kulipa ada badala ya kusubiri kulipiwa chama na wagombea uongozi huku akiwaasa viongozi wa chama hicho kushirikiana na jamii inayowazunguka.
Akifungua Kongamano hilo,mgeni rasmi,mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge aliwataka madiwani wa CCM kufanya shughuli za maendeleo badala ya kuendeleza majungu na kugombania vyeo.
Kwa upande wake katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Haula Kachwamba aliwataka watendaji wa serikali kushirikiana na viongozi wa CCM katika kutatua kero za wananchi.
Katika kongamano chama hicho kimepokea wanachama wapya 750 pamoja na waliokuwa makada wa CHADEMA na ACT Wazalendo.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,Kadama Malunde ametuletea picha 42 za matukio zilizojiri katika kongamano hilo
Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi ngazi ya mkoa na wilaya ya Shinyanga Mjini wakiwa wamesimama baada ya kuingia ukumbini kwa ajili ya kongamano kuadhimisha miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM. Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Viongozi wa CCM na wanachama wa chama hicho wakiwa wamesimama.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akifungua kongamano hilo.
Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge akizungumza wakati wa kufungua kongamano hilo.
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika kongamano hilo.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Gulam Hafeez Mukadam akiwasisitiza wanaCCM kushikamana.
Wazee wa CCM wakimsikiliza mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini.
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Gulam Hafeez Mukadam akizungumza ukumbini
Wafuasi wa CCM,Wanafunzi wa vyuo na shule za sekondari wakiwa ukumbini
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Haula Kachwamba akielezea kuhusu sera za CCM
Viongozi wa CCM wakimsikiliza Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoa wa Shinyanga Msanii Richard akizungumza katika kongamano hilo.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM mkoa wa Shinyanga Msanii Richard akizungumza katika kongamano hilo
Katibu wa siasa na uenezi wilaya ya Shinyanga Mjini Said Bwanga akifurahia jambo ukumbini
Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Charles Sangura akizungumza ukumbini
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Kongamano linaendelea
Kulia ni Katibu wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini, Charles Sangura akiwatambulisha waliokuwa makada wa CHADEMA na ACT Wazalendo (waliosimama kushoto) walioamua kuhamia CCM
Kushoto ni waliokuwa makada wa CHADEMA na ACT Wazalendo wakikaribishwa CCM. Katikati ni aliyekuwa mwenyekiti wa Baraza la wazee CHADEMA wilaya ya Shinyanga Mjini Robert Ng'welo akishikana mkono na Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge.Wa kwanza kushoto ni Owen Machiya Ndulu aliyekuwa mgombea udiwani kupitia CHADEMA
Aliyekuwa mwenyekiti wa wanawake CHADEMA kata ya Masekelo Fatuma Msafiri akirudisha kadi ya CHADEMA
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Haula Kachwamba akikabidhi kadi za CCM kwa wanachama wapya wa CCM ambapo CCM wilaya ya Shinyanga imepokea wanachama wapya 750
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Haula Kachwamba akiendelea kugawa kadi kwa wanachama wapya wa CCM
Zoezi la kukabidhi kadi za CCM likiendelea
Wanachama wapya wa CCM wakishikana mikono na viongozi wa CCM
Mwanachama mpya wa CCM akiwa ameshikilia kadi yake
Zoezi la kiapo likiendelea
Mwalimu Kija akielezea kuhusu dhana ya ujamaa na kujitegemea
Mzee Zamzam akichangia hoja wakati wa kongamano hilo
Mwanafunzi kutoka chuo cha Ufundi VETA Shinyanga akichangia hoja
Yusupuh John akichangia hoja ukumbini
Mwanafunzi wa chuo kikuu cha Ushirika MOCU akichangia hoja ukumbini
Mwanafunzi wa chuo cha ualimu Shycom Mwajuma Hamis akichangia hoja
Isaya Mwombeki kutoka kata ya Ndala akichangia hoja
Kongamano linaendelea
Kongamano likiendelea
Wanafunzi wa vyuo mbalimbali wakiwa ukumbini
Kongamano linaendelea
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Social Plugin