Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Shinyanga kimeadhimisha miaka 41 ya kuzaliwa kwa chama hicho kimkoa katika wilaya ya Kishapu na kuhudhuriwa na maelfu ya wanachama wa CCM na wananchi.
Akizungumza wakati wa sherehe hizo leo Jumapili Februari 4,2018, mgeni rasmi ,mwenyekiti wa chama hicho mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa alisema chama wana CCM wanasherehekea miaka 41 tangu kuzaliwa kwa CCM kwa sababu serikali inayosimamiwa na chama hicho imefanya mambo mengi mazuri ya kimaendeleo.
"Tangu chama kianzishwe nchi iko shwari,nchi inaongozwa kwa amani na tunazidi kuwaletea maendeleo wananchi kutokana na chama chetu kina misingi imara na wananchi wanakiamini",alieleza Mlolwa.
Katika hatua nyingine Mlolwa aliwataka viongozi wa chama hicho kuisimamia na kushirikiana na serikali katika kutatua kero za wananchi.
"Kila mmoja afanye kibarua alichopewa,wenyeviti wa vitongoji,mitaa,vijijini,madiwani na wabunge amkeni,msijifungie, nendeni kwa wananchi,fanyeni mikutano mkasikilize kero zao,haiwezekani wananchi wana kero halafu viongozi mpo tu",aliongeza Mlolwa.
Aidha aliwaasa wananchi kupenda kufanya kazi badala ya kulalamika kila siku kuwa maisha ni magumu 'vyuma vimekaza'.
Mlolwa pia alitahadharisha baadhi ya wanachama wa chama hicho wenye nia ya kuendekeza makundi ndani ya chama na kusisitiza kuwa hatakuwa tayari kuona mambo hayo katika uongozi wake.
Mwenyekiti huyo wa CCM pia aliwataka wanachama wa chama hicho kutoishi kinafiki kwa kusifiana tu hata kama mambo hayaendi sawa.
"Haiwezekani kila siku mtu anakuita wewe ni jembe,hakuna binadamu aliyekamilika,huwezi kuwa msafi kila siku,naomba pale tunapokosea tuambiane ili kurekebisha kasoro zinazojitokeza kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi",aliongeza Mlolwa.

Kilele cha maadhimisho ya sherehe hizo kimeenda sanjari na wanachama wa CCM kufanya shughuli mbalimbali ikiwemo upandaji miti wilayani Kishapu, kutoa msaada wa sabuni na viti vya wagonjwa katika hospitali ya wilaya ya Kishapu.
Chama hicho pia kimefanya mkutano mkuu wa CCM mkoa pamoja na mkutano wa hadhara katika uwanja wa SHIRECU uliopo katika mji wa Mhunze wilayani Kishapu.
Sherehe hizo pia zimeongozwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo msanii wa nyimbo za asili Mama Ushauri maarufu 'Full Melody Classic'
Sherehe hizo pia zimeongozwa na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali akiwemo msanii wa nyimbo za asili Mama Ushauri maarufu 'Full Melody Classic'
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog, Kadama Malunde ametuletea picha 72 za matukio yaliyojiri..Tazama hapa chini
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akipokelewa katika ofisi za CCM wilaya ya Kishapu kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM ambapo kimkoa maadhimisho hayo yamefanyika wilayani Kishapu
Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akiwaongoza viongozi wa CCM kwenda kusaini kitabu cha wageni katika ofisi ya CCM wilaya ya Kishapu
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akisalimiana na wanachama wa CCM nje ya ofisi za CCM wilaya ya Kishapu
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akikabidhiwa mche wa mti ili aupande katika ofisi za CCM wilaya ya Kishapu
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akipanda mti
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Gulam Hafeez Mukadam akipanda mti nje ya ofisi za CCM wilaya ya Kishapu
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akijiandaaa kupanda mti,kushoto ni katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Haula Kachwamba akipanda mti
Wanachama wa CCM wakipanda miti nje ya ofisi za CCM wilaya ya Kishapu
Msafara wa mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga ukielekea katika hospitali ya wilaya ya Kishapu kwa ajili ya kupanda miti na kutoa msaada wa sabuni na viti vya wagonjwa
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Boniface Butondo akipanda mti katika hospitali ya wilaya ya Kishapu
Katibu wa siasa na uenezi CCM mkoa wa Shinyanga Msanii Richard akiweka kopo la maji kwenye mti alioupanda huku mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM wilaya ya Shinyanga Mjini,Nayma Seif akimwagilia maji kwenye mti huo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Gulam na mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Shemahonge wakipanda mti katika hospitali ya wilaya ya Kishapu
Viongozi wa CCM mkoa wa Shinyanga wakipiga picha ya kumbukumbu katika hospitali ya wilaya ya Kishapu baada ya kupanda miti
Viongozi wa CCM na wanachama wa CCM wakipiga picha ya kumbukumbu katika hospitali ya wilaya ya Kishapu baada ya kupanda miti
Viongozi wa CCM wakiwa katika hospitali ya wilaya ya Kishapu wakati wa kugawa viti vya wagonjwa
Wanachama wa CCM wakiwa nje ya hospitali ya wilaya ya Kishapu wakati wa kukabidhi viti vya wagonjwa
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akizungumza wakati wa kupokea viti vya wagonjwa
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza wakati wa kugawa viti vya wagonjwa ambapo alisema chama hicho kitaendelea kuhakikisha huduma za afya zinaboreshwa katika wilaya ya Kishapu mkoa wa Shinyanga kwa ujumla
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza katika hospitali ya wilaya ya Kishapu.Kushoto ni Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Haula Kachwamba. Kulia ni katibu wa siasa na uenezi mkoa wa Shinyanga Msanii Richard
Wafanyakazi wa hospitali ya wilaya ya Kishapu wakiangalia viti vya wagonjwa vilivyotolewa na CCM mkoa wa Shinyanga.
Kulia ni Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akishikana mkono na mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Malisha Ntelezu.Mheshimiwa Nchambi alisema ametoa shilingi milioni 15 katika mfuko wa jimbo ili zisaidie kuboresha huduma za afya katika hospitali ya wilaya ya Kishapu
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akizungumza na wananchi katika mji wa Mhunze
Kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro,kulia ni mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhili Nkurlu na makada wa CCM wakiwa katika viwanja vya SHIRECU katika mji wa Mhunze
Picha ya kumbukumbu: Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Josephine Matiro na makada wa CCM
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akifungua mkutano wa wanachama wa CCM uliofanyika ukumbi wa SHIRECU katika mji wa Mhunze wilayani Kishapu kwa ajili ya kujadili masuala mbalimbali yanayohusu chama hicho
Mabala Mlolwa akizungumza na wanachama wa CCM na kuwasisitiza kuwa na maadili huku akiwataka viongozi wa wa chama na watendaji wa serikali kushirikiana katika kuwaletea maendeleo wananchi
Mabala Mlolwa akizungumza na wanachama wa CCM na kuwasisitiza kuwa na maadili huku akiwataka viongozi wa wa chama na watendaji wa serikali kushirikiana katika kuwaletea maendeleo wananchi
Mkutano unaendelea
Mabala Mlolwa akizungumza katika mkutano huo
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Haula Kachwamba akizungumza katika mkutano huo
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Haula Kachwamba akizungumza katika mkutano huo
Katibu wa CCM mkoa wa Shinyanga Haula Kachwamba akizungumza katika mkutano huo
Katibu wa siasa na uenezi CCM mkoa wa Shinyanga Msanii Richard akizungumza katika mkutano huo
Mwenyekiti wa UVCMM Baraka Shemahonge akizungumza katika mkutano huo
Mwenyekiti wa wazazi CCM Salum Simba akiwasalimia wanachama wa CCM
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Shinyanga Mjini Abuu Gulam Hafeez Mukadam akizungumza katika mkutano wa wanachama wa CCM uliofanyika katika ukumbi wa SHIRECU katika mji wa Mhunze
Wanachama wa CCM wakiwa katika mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM Kahama, Thomas Myonga akiwasalimia wanaCCM
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Mkuu wa wilaya ya Kishapu Nyabaganga Talaba akizungumza katika mkutano huo
Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kishapu Shija Malisha Ntelezu akiwasalimia wanachama wa CCM
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Wanachama wa CCM wakifuatilia matukio yaliyokuwa yanaendelea ukumbini
Mkutano unaendelea...
Wanachama wa CCM wakiwa ukumbini
Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akielezea jinsi wanavyoendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi katika kuwaletea maendeleo wananchi
Kushoto ni Mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akipokea hati ya pongezi kutoka kwa CCM wilaya ya Kishapu kutokana na mchango wake mkubwa katika kusaidia chama.
Cheti alichokabidhiwa mheshimiwa Nchambi
Mchungaji John Kingu kutoka kanisa la EAGT Maendeleo Kishapu akizungumza na kuomba wakati wa mkutano wa CCM
Wanachama wa CCM wakisali wakati wa mkutano huo wakiongozwa na Mchungaji John Kingu
Maombi yanaendelea ukumbini
Kushoto ni Msanii wa nyimbo za asili Mama Ushauri akishangilia wakati mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi akiingia katika eneo la mkutano wa hadhara wakati CCM ikidhimisha miaka 41 ya kuzaliwa kwa CCM.Katikati ni mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Shinyanga Baraka Semahonge akifuatiwa na mbunge wa Kishapu Suleiman Nchambi na wanachama wa CCM wakishangilia
Vijana wa Mama Ushauri 'Wacheza sarakasi' wakitoa burudani
Wanenguaji wa Mama Ushauri wakiingia uwanjani
Mama Ushauri akiimba na kucheza wimbo maalum kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 41 ya CCM
Mama Ushauri na wanenguaji wake wakitoa burudani katika mkutano wa CCM
Burudani kutoka kwa Mama Ushauri inaendelea
Wanenguaji wa Mama Ushauri wakionesha vipaji vyao vya kucheza muziki
Burudani kutoka Ngoma ya Majembe ikiendelea
Burudani inaendelea
Burudani inaendelea..vijana wa sarakasi kutoka kundi la B Boys nomaaa!!
B Boys wakitoa burudani ya kuruka juu
Meza kuu wakifuatilia burudani iliyokuwa inaendelea
Viongozi wa CCM wakiwa katika eneo la mkutano wa hadhara
Viongozi wa CCM wakiwa katika eneo la mkutano wa hadhara
Wafuasi wa CCM wakiwa eneo la mkutano
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akikabidhi kadi za CCM kwa wanachama wapya 1000 wa CCM kutoka wilaya ya Kishapu
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Mabala Mlolwa akimkaribisha aliyekuwa mwenyekiti wa Kijiji kupitia CHADEMA aliyeamua kurudisha kadi ya CHADEMA na kujiunga CCM
Kiapo kwa wanachama wa CCM kikiendelea
Wanachama wa CCM wakiwa katika mkutano huo
ANGALIA VIDEO SHOW YA MAMA USHAURI KWENYE SHEREHE ZA MIAKA 41 YA CCM