Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako pamoja na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ,Injinia Hamad Masauni wakimfariji Mama Mzazi wa marehemu Aqwilina jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar.
***
Mwanafunzi huyo wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji(NIT) amepoteza maisha baada ya kupigwa risasi Februari 16 mwaka huu eneo la Mkwajuni jijini Dar es Salaam wakati Polisi walipokuwa wakizuia maandamano ya chama cha CHADEMA.Kufuatia kifo cha Mwanafunzi huyo Serikali imesema itabeba jukumu la Mazishi yake.
Aidha Rais Dkt John Pombe Magufuli amesema amesikitishwa sana na kifo cha mwanafunzi huyo,Aqwilina Akwilini wa Chuo cha Usafirishaji (NIT).
"Natoa pole kwa familia,ndugu,wanafunzi wa NIT na wote walioguswa na msiba huu.Nimeviagiza vyombo vya dola kufanya uchunguzi na kuwachukulia hatua za kisheria waliosababisha tukio hili",Ilisema sehemu ya taarifa yake iliyotolewa mapema leo.
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi Prof Joyce Ndalichako (tatu kulia) akiwafariji Mama Mzazi wa marehemu Aqwilina pamoja na ndugu jioni ya leo Mbezi Kimara jijini Dar
Mama wa Marehemu Akwiline akilia kwa uchungu mara baada ya kuona viongozi wa Waandamizi wa serikali walipofika nyumbani kwake,Mbezi Kimara jioni ya leo kwa lengo la kutoa pole na kufahamu taratibu mbalimbali za msiba huo.
Social Plugin