POLISI ALIYEUA KWA RISASI KWENYE MAANDAMANO ATUPWA JELA MAISHA

Mahakama ya kijeshi nchini Kongo imemfunga kifungo cha maisha jela ofisa wa polisi aliyemuua kwa kumpiga risasi mshiriki wa maandamano ya kumpinga Rais Joseph Kabila.

Ofisa usajili katika mahakama ya kijeshi Kaskazini Magharibi mwa DRC aliliambia shirika la AFP Ofisa wa polisi Agbe Obeid amehukumiwa kifungo cha maisha gerezani kwa kumpiga risasi kwa karibu na kumuua Eric Boloko Jumapili, Februari 25, eneo la Mbandaka.

Maandamano hayo yalipangwa kutokana kwanza na kushindwa kwa Kabila kung’atuka baada ya muhula wake wa pili wa miaka mitano kumalizika Desemba 2016 na pili kuchelewa kwa uchaguzi ambao sasa umepangwa kufanyika mwisho wa 2018.

Boloko alikuwa mmoja wa watu wawili walioripotiwa kuuawa na vikosi vya usalama wakati wa maandamano ya mwishoni mwa wiki katika miji ya DRC yaliyozuiwa na utawala wa Kabila lakini yaliungwa mkono na Kanisa la Katoliki lenye ushawishi mkubwa.

Maandamano yaliyofanyika Mbandaka Desemba 31 na Januari 21 yaliyoandaliwa na wasomi wa kanisani yalisababisha watu 15 kuuawa baada ya kumiminiwa risasi na vikosi vya usalama.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post